Home VIWANDA Wanawake wataka kiwanda cha kusindika nafaka

Wanawake wataka kiwanda cha kusindika nafaka

0 comment 102 views

Wanawake wa kikundi cha Wamsoe kilichopo kijiji cha Lerang’wa kata ya Olmolog wameitaka serikali kuwapa ushirikiano ili waweze kujenga kiwanda cha kusindika mazao ya chakula hususani nafaka.

Mwenyekiti wa kikundi hicho Frida Silayo, ameeleza kuwa kikundi hicho kilianza na wanawake 198 na sasa wameongezeka na kufikia 300 ambapo kata ya utendaji wapo watu watano na  upande wa halmashauri wapo 40.Wanachama wa kikundi hicho wanafanya kilimo, ujasiliamali,  ushonaji wa shanga za kimasai,wanaandaa vitambaa vya batiki, ununuzi wa mazao na kufanya uwekezaji wa hisa ili kuondokana na mazoea yanayohusu utegemezi kwa waume zao(mfumo dume).

“Huku tunalima zaidi na wanawake wengi ni wazalishaji wa mazao, tulikuwa hatuna pa kuhifadhia, lakini sasa ghala limekamilika tutapiga hatua. Serikali na wadau watusaidie tupate kiwanda cha kusindika nafaka “ amesema Mwenyekiti huyo.

Pia aliongezea kuwa, kukamilika kwa ghala hilo kutawasaidia kuacha kuuza mazao yao kwa hasara kwani walikuwa wakiuza mazao kama mahindi gunia moja kwa 30,000 na maharage 60,000 kwa wakenya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la maendeleo FEESO Lomayani Komolo, ameeleza kuwa shirika hilo hutoa msaada kwa wajasiliamali ambao wameshaanza kutekeleza mradi ambao wanautaka na hivyo wananchi hao walijenga msingi wa ghala hilo kwa shilingi milioni 12 huku shirika hilo likikamilisha ghala hilo kwa milioni 71

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter