Home VIWANDA Ujerumani yaahidi kiwanda

Ujerumani yaahidi kiwanda

0 comment 127 views

Kupitia mazungumzo yaliyofanywa kwa njia ya simu, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amemuahidi Rais Magufuli kuwa, nchi hiyo ipo tayari kukuza mahusiano yake na Tanzania ili kusaidia jitihada za kuimarisha uchumi. Kansela huyo amesema Ujerumani itawaleta wawekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo watakaojenga kiwanda cha uzalishaji mbolea ambacho kitakuwa namba moja kwa ukubwa barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu, Kansela Merkel amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli katika kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kupambana na rushwa na kuboresha miundombinu. Ameongeza kuwa, Ujerumani imedhamiria kuunga mkono mchakato wa ujenzi wa viwanda nchini Tanzania na kwamba, kiwanda hicho cha mbolea kitasaidia taifa kuongeza kipato na vilevile kuimarisha kilimo.

Kwa upande wake, Rais Magufuli ameshukuru kiongozi huyo kwa kuweka wazi nia yake ya kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania na kumueleza kuwa, Tanzania itahakikisha inaweka mazingira rafiki ya katika maeneo yote ya ushirikiano hususani uwekezaji na biashara. Rais Magufuli pia amemhakikishia Kansela Merkel kuwa Tanzania itadumisha ushirikiano uliopo kwa manufaa ya nchi zote mbili.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter