Home VIWANDA TPSF yachochea uanzilishaji wa viwanda vya gesi

TPSF yachochea uanzilishaji wa viwanda vya gesi

0 comment 133 views
Na Mwandishi Wetu

Katika uzinduzi wa maonyesho ya mitambo na mashine za uchimbaji gesi, umeme na mafuta jiji Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye amewataka wadau wa mitambo ya rasilimali hizi kujenga viwanda hapa nchini

Simbeye ameyasema hayo katika uzinduzi wa maonyesho haya ambayo yameshirikisha mataifa zaidi ya 25 kati yao yakiwemo Uturuki, Misri, India na Japan huku akisisitiza wadau wa sekta hii kutoleta tu bidhaa kutoka nje bali wafikirie kuanza kujenga viwanda ili baadhi ya bidhaa ziweze kutengezwa hapa nchini kwa kutumia gesi asilia.

Ameongeza kuwa iwapo serikali ikizidi kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara, basi miradi mikubwa itafanyika na kuwanufaisha watanzania wengi. Hadi kufikia sasa, zaidi ya futi 57 trilioni za ujazo wa gesi asilia zimegundulika na taasisi na makampuni zaidi ya 70 tayari yameunganishwa kwenye matumizi haya jijini Dar es salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter