Home BIASHARA M-pesa yawapa unafuu wasafiri wa anga

M-pesa yawapa unafuu wasafiri wa anga

0 comment 112 views

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), wametangaza ofa ya punguzo labei kwa asilimia15 kwa kila mteja atakaye nunua tiketi kutoka shirika hilo kupitia huduma ya M-Pesa, Ofa hii ni kuanzia tarehe 1 mwezi wa nane mpaka tarehe 1 Disemba mwaka huu. Ofa hii ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Balozi wa Uturuki nchini,Ali Davutoglu na Mkurugenzi wa M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni.

Akizungumza katikauzinduzihuo, Mkurugenzi wa  Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon,M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni , alisema ubia huo umelenga kuchochea malipo ya kifedha kupitia njia za kidijitali kwa kuwawezesha wateja wao kufanya malipo kwa urahisi wanaponunua tiketi za ndege kutokashirika la ndege la Uturuki (Turkish Airline) na kuelekea sehemu yeyote duniani wakianzia safari zao Tanzania.

“Tuna wajibu wa kutengeneza bidhaa na huduma za kifedha ambazo zinakidhi mahitaji ya watu binafsi nabiashara, kama shirika la ndege la Ututurki. Ulipaji kupitia M-Pesa ni njia rahisi zaidi ya kufanya malipo; wateja wetu watafurahia faida za kulipia tiketi zao mda wowote na wakati wowote kupitia M-Pesa ukizingatia wanazawadiwa pindi wanapofanya malipo”, alisema Arjun

Akizungumza juu ya ofa hiyo Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, aliwapongeza Vodacom kwa kutumia teknolojia yao kuchochea huduma za kidijitali nchini. Sahin aliongeza kuwa huduma hii ni yakipekee kwa wafanyabiashara nchini Tanzania kulipia usafiri wa ndege kwenda Uturuki au maeneo 312 ambayo ndege zake zinafika, pamoja na kufaidika kibiashara na kujionea vitu ambavyo nchi zingine zinafanya (exposure).

Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu (katikati) na Mkurugenzi wa M-commerce wa Vodacom Tanzania Epimack Mbeteni (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon (wa pili kulia), wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, ( wapili kushoto) akielezea punguzo la bei kwa asilimia 15 kwa wateja pindi wanaponunua tiketi ya kusafiria kutoka shirika la ndege la Uturuki (Turkish airline) kupitia huduma ya M-Pesa kuanzia tarehe 1 Agosti mpaka Disemba Mosi mwaka huu. Ofa hiyo ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam jana.

“Wateja ambao watanunua tiketi za shirika la ndege la Uturuki kuanziatarehe moja mwezi wa nane mpaka Disemba mosi watapata, sio tu pungufu ya bei kwa asilimia 15% kwa safari zote zinazoanzia Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro, bali pia watafurahia huduma zinazotolewa kwa masaa 24 kutoka kwa watoa huduma wetu nchini kote. Napenda kuwahimiza wafanyabiashara, watalii na wateja wetu wote kutumia fursa hii,” alisistiza Sahin.

Shirika la ndege la Uturuki linaruka kwenda maeneo 312 katika nchi 126 duniani na ofa hii inahusu safari zote zinazoanzia nchini Tanzania kuelekea maeneo hayo.

Vodacom Tanzania Plc inaendeleza nia yake ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anafaidikia na huduma bunifu zitokanazo na mtandao wa simu, vile vile kufungua fursa za kidijitali kwa Watanzania hasa wakati huu tukielekea kuinua uchumi wa nchi kuwa wa kati ifikapo mwaka 2025.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter