Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Biashara kubwa zaidi mtandaoni hizi hapa

Biashara kubwa zaidi mtandaoni hizi hapa

0 comment 101 views

Ulimwengu wa teknolojia umekuja na fursa mbalimbali za ajira na katika nyakati hizi ambazo soko la ajira limeendelea kuwa gumu, vijana wengi wametumia fursa hii kujiingizia kipato na kumudu gharama za maisha.

Badala ya kusubiri kuajiriwa, unaweza kufanya vitu hivi na kutengeneza kipato. Teknolojia imewezesha uwepo wa fursa mbalimbali za ajira na biashara na hii imekuwa mkombozi wa wengi.

Hizi ni biashara kubwa zaidi unazoweza kufanya mtandaoni hivi sasa:

Tovuti

Kuna tovuti chache sana zilizopo kwa lugha ya kiswahili na hiyo peke yake ni fursa tosha kwako kuanzisha tovuti na kutengeneza kipato. Kama unafikiria kufanya hivi, ni muhimu kuhakikisha kuwa unajua nini hasa wasomaji wako wanataka. Weka jitihada kubwa katika kuwafikia wasomaji wengi na kuwa na idadi inayoridhisha ili kuvutia matangazo kutoka kwa wdau mbalimbali.

Utafutaji masoko kwa niaba ya makampuni (Affiliate Marketing)

Japokuwa ni vigumu kwa kampuni kukosa kitengo cha masoko, bado kuna fursa nzuri ya kujiajiri kutafuta matangazo kwa ajili ya makampuni mbalimbali ikiwa una idadi kubwa ya wafuatiaji na ushawishi wako mtandaoni na katika jamii ni mkubwa. Ikiwa una vitu hivyo basi unaweza kugeuza ushawishi wako kama ajira kwa kutafuta wateja kwa ajili ya makampuni. Jambo la muhimu katika ajira hii ni kuhakikisha kuwa unakuwa uaminifu na unawasaidia wateja kuelewa bidhaa kwa undani. Unapojenga mahusiano mazuri na ya muda mrefu na wafuatiaji/wateja wako, inakuwa rahisi kuwauzia bidhaa au huduma mbalimbali.

Dropshipping

Hakuna neno rasmi la kiswahili la biashara hii lakini kwa ufupi Dopshipping ni kitendo cha kuwanunua wateja bidhaa mtandaoni. Ikiwa wewe ni mfanyabiashara ambaye kwa asilimia kubwa unategemea mitandao, bila shaka umewahi kukutana na watu wanaofanya biashara hii kwa kuwa wafanyabiashara walio wengi wanakutana na vikwazo kama njia rahisi za malipo na usafirishaji, hali inayowafanya kushindwa kuagiza bidhaa wenyewe moja kwa moja. Unaweza kununua bidhaa moja kwa moja katika mitandao kama Amazon na Ebay na kuhakikisha mzigo unamfikia mteja moja kwa moja pasipo yeye kuwasiliana na kampuni husika. Biashara hii inahitaji uaminufu wa hali ya juu pamoja na jitihada za kufanya kazi bila kuchoka hususani kama ndio kwanza unaanza.

Youtube 

Sawa na kuanzisha tovuti, kabla hufungua chaneli yako ya Youtube ni muhimu kujua ni nini hasa unataka kufanya kwani itakusaidia kujipanga vizuri zaidi. Watu wengi hushindwa katika hili kutokana na kukosa muelekeo sahihi na hivyo kupoteza wafuatiliaji kirahisi. Ni muhimu kuwa na mpango ambao utakuongoza na kukusaidia kufanikisha malengo yako. Youtube imesaidia watu wengi kujiajiri na kutengeneza kipato cha uhakika hivyo ni kiyu ambacho kinawezekana kabisa ukijipanga vizuri na kufanya kazi kwa bidii.

Social Media Influencer

Ikiwa wewe ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijamii na una idadi nzuri wa wafuatiliaji, basi unaweza kutumia njia hiyo kujiingizia kipato kwa kushirikiana na makampuni makubwa kutangaza bidhaa au huduma wanayotoa. Pamoja na hayo, unaweza kutumia ukurasa wako kwa ajili ya matangazo na kutengeneza kipato kizuri. Vijana wengi wameendelea kujiajiri kwa kupitia mitandao kama Instagram. Ikiwa una idadi kubwa ya wafuatiliaji, hii ni fursa nzuri kwako kutengeneza fedha na kufanya kazi na biashara mbalimbali.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter