Home BENKI AfDB yapongeza ukuaji uchumi

AfDB yapongeza ukuaji uchumi

0 comment 102 views

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB), Dk. Akinwumi Adesina ameipongeza Tanzania kwa kukuza uchumi wake kwa asilimia 7 na kuwa katika kundi la nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi. Dk. Adesina ametoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli jijini Dar es salaam ambapo mbali na kumpongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kuwapigania watanzania, pia amesisitiza kuendelea na kasi hiyo ili kuzidi kuimarisha uchumi wa nchi.

Aidha, Tanzania kuendelea kushirikiana na nchi jirani ikiwemo Uganda katika mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi lenye urefu wa kilomita 1,443 kutoka Hoima Uganda hadi mkoani Tanga. Rais huyo ameeleza kuwa AfDB hiyo ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye masuala ya masoko ya mazao yanayozalishwa hapa nchini, na mpaka sasa benki hiyo imefanikiwa kufadhili miradi inayogharimu Sh. 4.55 trilioni.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko zenye urefu wa kilometa 110 na vilevile ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato.

Kwa upande wake, Rais Magufuli amesema benki hiyo imekubali kutoa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Mpanda-Tabora (kilometa 359), mradi wa mabasi yaendayo haraka awamu ya pili (BRT) kati ya Mbagala na Kariakoo jijini Dar es salaam, na kujenga njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 400 kati ya Sumbawanga, Mpanda, Kigoma na Nyakanazi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter