Banc Abc Tanzania imewapa sapoti wanawake nchini kwa kudhamini mkutano wa chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) ambao huwakutanisha zaidi ya wanawake 250 kutoka Tanzania bara na visiwani.
Mkutano huo ambao hufanyika kila mwezi ulidhaminiwa na benki hiyo ambapo mkurungezi wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara Joyce Malai alisisitiza kuwa benki hiyo inatambua umuhimu wa wanawake katika kukuza uchumi wa nchi hivyo itaendelea kushirikiana nao kwa kuwapa huduma rafiki ikiwemo huduma iliyofunguliwa hivi karibuni ya Yuan pre-paid visa card inayomuwezesha mteja kubadilisha fedha na kufanya malipo kwa fedha za kigeni ikiwemo china.
Benki hiyo ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara ambayo imejiorodhesha katika soko la hisa la London imeahidi kuwasaidia wafanyabiashara hao wanawake hususani wanaposafiri kwenda kufata bidhaa hasa china kwa kuwawezesha kufanya malipo kwa fedha ya nchi aliyopo ikiwemo fedha ya china kwa thamani ile ile.
Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa Twcc Mwajuma Hamza aliishukuru benki hiyo huku akiwaahidi ushirikiano ikizingatiwa Twcc ni chama kinachounganisha wanawake kwenye sekta zote na mikoa yote Tanzania bara na visiwani.