Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO JPM atoa vitambulisho kwa wamachinga, aagiza wasisumbuliwe

JPM atoa vitambulisho kwa wamachinga, aagiza wasisumbuliwe

0 comment 141 views

Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amezindua vitambulisho 670,000 maalum kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo ili kuzitambulisha biashara zao na kuhakikisha hawasumbuliwi. Rais Magufuli amegawa vitambulisho hivyo katika mkutano wake na viongozi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) pamoja na wakuu wa mikoa ambapo ameeleza kuwa, vitambulisho hivyo ni maalum kwa wafanyabiashara ambao mitaji yao haijafikia Shilingi milioni nne. Rais Magufuli amekabidhi vitambulisho hivyo kwa wakuu wa mikoa na kuagiza wakawapatie wafanyabiashara katika maeneo yao na kutaka wasisumbuliwe na mtu yeyote.

“Nimefikia hatua ya kutoa vitambulisho hivyo mimi mwenyewe kwa sababu nimeona mamlaka husika inachelewesha na wafanyabiashara wadogo wanaendelea kusumbuliwa. Vitambulisho hivi navitoa bure ila wafanyabiashara watachangia 20,000 kila mmoja, kama kurudisha gharama ya utengenezwaji wake ili fedha hizo zikatumike kutengenezea vitambulisho vingine na kianze kutumika mara tu anapokipata. Kama vitambulisho hivi navitoa mimi mwenyewe sijaona mtu wa kuwasumbua, na mfanyabiashara mwenye mtaji wa chini ya Sh 4,000,000 na ana kitambulisho nasisitiza asisumbuliwe”. Ameeleza Rais Magufuli.

Katika vitambulisho hivyo 670,000, kila mkuu wa mkoa atapatiwa vitambulisho 25,000 ambavyo atagawa kwa wafanyabiashara wa maeneo yao ambapo fedha watakazopewa watatakiwa kulipa TRA. Pamoja na hayo, Rais Magufuli ameshauri wafanyabiashara watakaopata vitambulisho hivyo kuvitumia kwa matumizi yao na sio kuwafanyia biashara wafanyabiashara wakubwa.

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter