Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Ushuru waporomoka Machinga Complex

Ushuru waporomoka Machinga Complex

0 comment 138 views

 

Na Mwandishi wetu

Ushuru katika jengo la Machinga Complex umeendelea kushuka katika siku za hivi karibuni mpaka kufikia Sh. 600 milioni ambapo hapo awali soko hilo lilikuwa likikusanya ushuru hadi Sh, 750 milioni kwa mwaka. Hayo yamesemwa na Meneja wa soko hilo Ananias Kamundu huku akidai kuwa chanzo cha kuporomoka kwa ushuru unaokusanywa ni wafanyabiashara kupungua katika jengo hilo.

Kamundu amefafanua kuwa  baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa na mabanda katika jengo hilo wamehamia pembezoni mwa barabara pamoja na maeneo mengine ambayo hapo mwanzo yalizuiliwa na mamlaka kutumika kwa ajili ya shughuli za kibiashara. Meneja huyo ameongeza kuwa kitendo hicho kimepelekea soko hilo kupoteza mapato

Desemba mwaka jana, Rais Magufuli alipiga marufuku wakuu wa mikoa, wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuwafukuza wafanyabiashara ndogondogo mijini, hivyo wafanyabiashara katika jengo la Machinga Complex wamekuwa wakihamishia biashara zao katika sehemu hizo kwani wana ruksa ya kufanya hivyo bila kudaiwa ushuru na kusumbuliwa na mgambo wa jiji.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter