Home BIASHARA China kufungua zaidi soko lake kwa bidhaa za Tanzania

China kufungua zaidi soko lake kwa bidhaa za Tanzania

0 comment 112 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa China Xi Jinping ambopo Rais Jinping amemuahidi Rais Samia kuunga mkono jitihada za serikali yake katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Rais Jinping ameahidi kuwa China itafungua zaidi soko lake kwa bidhaa za Tanzania pamoja na kuongeza uwekezaji hususani katika sekta ya viwanda.

Nchi hizo mbili zimekubaliana kukuza ushirikiano katika Nyanja za uchumi, utamaduni na ushirikiano wa kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, katika mazungumzo hayo, Rais Samia ametoa salamu za pongezi kwa Chama cha Kikomunisti China (CPC) kwa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake na amaahidi kudumisha uhusiano kwa kindugu na kihistoria uliopo kati ya hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter