Home BIASHARA Kuna sababu ya kuokoa biashara inayofilisika?

Kuna sababu ya kuokoa biashara inayofilisika?

0 comment 124 views

Inawezekana kuokoa biashara ikiwa imefilisika. Hata hivyo inatakiwa kuchunguza kama biashara inafaa kuokolewa au la. Kwa ujumla unatakiwa kufikiria kuiokoa biashara ikiwa una uhakika kuwa biashara hiyo inaweza kuleta faida na kurudisha mali zenye thamani zaidi ya madeni inayodaiwa. Kwa kufanya uchunguzi utajua biashara imefilisika kwa kiasi gani na maamuzi gani unaweza kuchukua.

Mambo ya kuzingatia:

Jambo la msingi ni kujua kwanini biashara inapoteza fedha kabla hujaamua kuwa imefilisika. Unatakiwa kutambua kwanini biashara haina faida. Kwa mfano, biashara inaweza kuathiriwa na hali ya hewa kama mafuriko au mfanyakazi muhimu akaacha kazi na kusababisha biashara kuyumba. Ikiwa kuna namna ya kusuluhisha mambo kama haya basi unaweza kutafuta suluhisho la kuokoa biashara yako. Lakini kama sababu inayopelekea biashara isiendelee ni kushindwa kutengeneza faida basi hakuna msingi kuiendeleza kwa sababu hakuna maana ya kuendelea nayo kama hakuna faida.

Kujua thamani ya jumla ya mali zako kutasaidia kujua kama kuna umuhimu wa kuokoa biashara au la baada ya kufilisika. Pia unatakiwa kulinganisha mali zako za biashara na madeni unayodaiwa. Anza kwa kuorodhesha mali za biashara na thamani ya kila mali.

Tathmini madeni yako. Ili kulinganisha mali na madeni ya biashara unatakiwa kuorodhesha madeni yako yote na kuwa na uhakika na orodha hiyo kuwa ni sahihi. Madeni yanaweza kuwa mikopo, vifaa ambavyo havikulipwa, mzigo wa biashara ambao haukulipwa n.k. Ikiwa mali zitazidi madeni basi biashara inastahili kuokolewa. Hata hivyo unashauriwa kuachana na biashara husika ikiwa madeni yamezidi mali ulizonazo.

Unatakiwa kujua kama mikopo ilichukuliwa kama biashara au mtu binafsi. Kuingiza mali binafsi katika mikopo ya biashara kunaweza kuathiri maisha kwa ujumla ndio maana ni muhimu kutofautisha masuala binafsi na yale ya kibiashara.

Ikiwa unataka kuokoa biashara yako kwanza unatakiwa kuwasiliana na mwanasheria anayehusika na biashara ili uweze kujua maamuzi sahihi unayotakiwa kuchukua na kama itahitajika kuhusisha masuala ya kisheria ili kuokoa biashara. Kuna biashara ambazo zilifilisika na kuokolewa kisha kupata mafanikio makubwa. Jambo la muhimu ni kutumia njia sahihi kutatua changamoto zilizopo.

Kama utatengeneza faili la kufilisika kwa biashara ni vyema ukamuhusisha mwanasheria ili ujue kama una vigezo vya kufaili ripoti hiyo. Mwanasheria anatakiwa kufuatilia mchakato wote na kuhakikisha ripoti inawasilishwa kwa hakimu.

Kuna kitu kinaitwa “automatic stay” hii humsaidia mfanyabiashara pale ripoti yake ikikubaliwa. Ikiwa mfanyabiashara ameamua kuokoa biashara yake kwa kufaili ripoti ya kufilisika mahakamani na mahakama ikakubali ripoti hiyo, basi watu wote wanaoidai biashara husika watatakiwa kuacha kuwasiliana na mmiliki wa biashara husika kuhusu madeni anayodaiwa kwa kipindi chote biashara inapojaribu kujiokoa, mkopeshaji yoyote atakaekiuka hilo basi hutakiwa kumlipa mmiliki fidia.

Pia mabadiliko yoyote wakati biashara inajaribu kujiokoa hutakiwa kuwasilishwa mahakamani. Kwa mfano kama biashara inatengeneza faida basi mahakama inatakiwa kujua ili kufanya mabadiliko.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter