Maboresho ya teknolojia yameendelea kurahisisha shughuli za wafanyabiashara duniani ikiwa ni pamoja na swala la utafutaji masoko kwa kupitia mitandao ya kijamii. Si kila mtu ana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kukuza mapato katika biashara kwa sababu watu hususani watu wazima wamejiwekea kuwa mitandao ya kijamii inawahusu vijana zaidi kitu ambacho si kweli.
Ikiwa hufurahishwi na mwenendo wa biashara yako na hutumii mitandao ya kijamii kuitangaza biashara yako, muda umefika kubadilisha hilo ili kuleta mapinduzi katika biashara yako.
Mambo matatu ya kuzingatia kuhusu mkakati wa vyombo vya habari vya kijamii:
Chagua majukwaa sahihi.
Facebook, Pinterest, Tumblr, Instagram, na Twitter ni baadhi ya majukwaa maarufu yaliyotumiwa sana siku hizi. Ikiwa unawajua wateja wako ni rahisi kujua ni mitandao ipi ya kuzingatia. Hivyo jitahidi kuongeza kasi katika majukwaa yanayofurahishwa na mikakati ya biashara yako. Kwa mfano watumiaji wa Twitter huhitaji majibu ya haraka 24/7 ikiwa biashara yako haifanyi kazi masaa 24 basi twitter si jukwaa lako sahihi.
Si lazima uwe katika mitandao yote. Ili kutengeneza thamani inayoeleweka jaribu tu kuangalia ni mitandao gani wateja wako wanajihusisha nayo zaidi baada ya kujua hilo tengeneza maudhui yanayoendana na mtandao husika.
Jiwekee malengo
Kila biashara huwa na malengo tofauti. Lakini kila biashara inayofanyika katika mitandao lazima huwa inakuwa na malengo yanayofanana ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya wateja inatokea wapi, je foleni katika tovuti ni kubwa kiasi gani, kizazi gani kinaongoza kuiungisha biashara husika, manunuzi ya mtandao, mrejesho kutoka kwa wateja nk hivyo ni muhimu kujua unayakabiri vipi mambo kama haya ili kufikia malengo elekezi ya biashara yako.
Siku zote wateja wengi hufurahishwa na majibu ya haraka kutoka kwa wafanyabiashara hii hupelekea wateja hao kuwaambia na watu wengi kwenda kununua bidhaa kupitia akaunti husika. matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ni moja ya mikakati ya biashara inayoweza kupelekea kuleta uelewa kwa wateja, uaminifu na mapato. Hivyo jitahidi kuunda mkakati wa kutathmini athari nzuri na mbaya.
Tengeneza mipango sahihi wa maudhui
Jitahidi kuwa na mpango sahihi wa maudhui yako unayotuma katika mitandao ya kijamii. Jiulize maswali kama, “Ni sababu gani ninaweka maudhui haya?” Uumbaji wa maudhui ya kimkakati husaidia kuunganisha timu yako na mkakati wa biashara yako yote. Unatakiwa kujua ni mara ngapo utakuwa unaweka maudhui mapya katika akaunti yako na kutathmini mafanikio ya kuweka maudhui hayo. Baada ya kujua ni mtandao upi wa kijamii unaleta mrejesho mzuri zaidi basi tengeneza mpango madhubuti wa kuboresha maudhui utakayokuwa unaweka katika mtandao husika.
Ni muhimu kuchapisha maudhui muhimu na yenye kuvutia kwenye vyombo vya habari vya kijamii, mara kwa mara. Maudhui bora huwashawishi watu kujihusisha zaidi na brand yako, mara kwa mara.