Home BIASHARA Tanzania kuunga mkono biashara huru AU

Tanzania kuunga mkono biashara huru AU

0 comment 132 views

Mwakilishi wa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mtangamano wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Thomas Mcharo amesema Tanzania ipo kwenye mchakato wa kusaini maridhiano ya biashara huru kwa wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kuwa lengo la biashara ya pamoja kwa jumuiya hizo ni kuinua uchumi. Mcharo ambaye pia ni Afisa Biashara ameeleza kuwa kuelekea uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda, kufanya biashara huru kutasaidia taifa kuchochea uzalishaji zaidi viwandani na vilevile itapekelea uwepo wa masoko ya kutosha.

“Awali tulikuwa tukitegemea soko la EAC na SADC, ila kuwepo kwa makubaliano haya ya Umoja wa Afrika tutajinufaisha zaidi kiuchumi, kutokana na uzalishaji wa bidhaa kuongezeka pamoja na kutanuka kwa soko”. Amesema Afisa huyo.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa bidhaa na biashara wa AUC (Kamishenni ya Umoja wa Afrika) Dk. Halima Noor amesema nchi wanachama 52 kati ya 55 zilizopo AU tayari zimesaini mkataba wa kuridhia biashara huru kwa pamoja.

Imeelezwa kuwa, biashara hiyo ina hatua tatu ambapo asilimia 90 ya bidhaa zilizopo kwa wanachama hazitatozwa ushuru kwenye vituo vya forodha, asilimia 7 hazitofunguliwa na asilimia 3 watalipa ushuru kwa awamu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter