• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Monday, October 2, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Umuhimu wa kujiunga na VICOBA

Patricia Richard by Patricia Richard
May 16, 2018
in FEDHA
0
Share on FacebookShare on Twitter

Bila shaka kwa wengi neno Vicoba sio neno jipya. Limekuwa linatumika kwa muda mrefu katika sehemu mbalimbali ndani ya jamii zetu. Kwa kirefu Vicoba inafahamika kama ‘Village Community Bank’ ikiwa ni kikundi cha watu kati ya 15 hadi 30 wanaofahamiana na kukubaliana katika malengo na katiba, ambao hukutana katika muda uliopangwa ili kupata huduma ya mafunzo ya ujasiriamali na huduma ya fedha. Hapo chini ni baadhi ya sababu za kujiunga na makundi haya.

Vicoba imekuwa kama darasa huru kwa watanzania wengi. Uwepo wa vikundi hivi umesaidia wananchi kujiamini, kujitambua na kuelewa uwezo walionao, hivyo kutumia uwezo huo katika kujiingizia kipato. Kupitia Vicoba watu wengi wamefanikiwa kuondokana na umaskini kwa kupata mafunzo mbalimbali hivyo kutumia fursa hiyo kujikomboa na kutumia uwezo walionao kujiingizia kipato.

Shughuli za ujasiriamali pia zimeendelea kukua kwa kasi kwa kupitia Vicoba. Makundi haya ya watu yamesaidia kuibua mamia ya wajasiriamali wapya na hivyo yamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi na ukuaji wetu wa uchumi. Kujiunga na Vicoba kunampa fursa mjasiriamali kukutana na wazoefu zaidi ambao wanaweza kuwa washauri na waalimu kwake hivyo kupelekea ujuzi wake kuongezeka. Vicoba pia ni nafasi nzuri ya wajasiriamali kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa au huduma wanazotoa.

ADVERTISEMENT

Aidha kwa kujiunga na Vicoba unapata fursa ya kukutana na watu mbalimbali kutoka serikalini, sekta binafsi, wabia wa vicoba wakati wa mafunzo, mikutano, semina, makongamano, uzinduzi na sherehe mbalimbali hivyo ni nafasi nzuri ya kubadilishana ujuzi, mbinu na uzoefu katika shughuli za kifedha, kiuchumi, kijamii na mfumo mzima wa maisha ya kila siku na maendeleo endelevu ndani na nje ya nchi. Unapata nafasi nzuri ya kujenga mahusiano ya kibiashara na watu mbalimbali ndani ya muda mfupi. Kupata nafasi ya kuona wengine wanachokifanya pia bila shaka kutakuhamasisha na wewe kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo uliyojiwekea.

Kupitia Vicoba mwanachama anakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupata mikopo yenye masharti nafuu. Sote tunajua kuwa taasisi na mashirika mbalimbali hayatoi mikopo kwa urahisi lakini kwa kuwa mwanachama wa Vicoba, unaweza kupatiwa mikopo kwa urahisi zaidi hivyo kufanikisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambayo ingeweza kukwama bila ya mikopo hiyo..

Taasisi na mashirika mbalimbali kutoka ndani na hata nje ya nje yanafikia Vicoba kwa urahisi ukilinganisha na watu ambao hawajajiunga na  makundi haya. Taasisi hizi hutoa misaada kwa Vicoba kwa wingi zaidi kwani inakuwa rahisi kwa wao kuona kile wanachofanya na pia jinsi gani wanaweza kuwasaidia. Tofauti na yule ambaye hajajiunga na vikundi hivi, mashirika yanayoweza kumfikia yanakuwa machache hivyo hupelekea kutumia muda mrefu kutafuta msaada.

Mfumo huu umekuwa na mafanikio makubwa katika kupunguza umaskini kwenye maeneo mbalimbali ambayo tayari unafanya kazi. Ushirikishwaji katika kuanzisha na hata kusimamia vikundi hivi umezidi kuwavutia wananchi wengi. Hivyo basi elimu zaidi  kuhusu umuhimu wa vikundi hivi itolewe kwa wananchi hapa nchini.

Tags: fedhamikopoujasiriamaliVICOBA
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post

Unafahamu soko lako vizuri?

Discussion about this post

Habari Mpya

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

September 14, 2023

Exim kulinda maslahi watumiaji huduma za bima

September 26, 2023
Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande.

Tanzania yapiga hatua utakatishaji fedha

September 12, 2023
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Picha| Ikulu

Tutawaunganisha wakulima na soko: Rais Samia

September 11, 2023

Mbaazi yaleta neema kwa wakulima 2023

September 7, 2023

Bei za mafuta zapanda tena Tz

September 6, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

by Pesatu Reporter
September 14, 2023
0

Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa asali barani Afrika na inashika nafasi ya 14 dunia. Ethiopia, ndio nchi...

Exim kulinda maslahi watumiaji huduma za bima

by Pesatu Reporter
September 26, 2023
0

Benki ya Exim imezindua ushirikiano wa kimkakati na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na kufanya mafunzo ya...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In