Home BIASHARAUWEKEZAJI Bilioni 116 kumaliza tatizo la maji

Bilioni 116 kumaliza tatizo la maji

0 comment 116 views

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ametoa ahadi ya uhakika wa majisafi na salama kwa wakazi wa wilaya ya Bagamoyo kufuatia hatua nzuri za utekelezaji wa miradi ya maji katika wilayani humo. Waziri Mbarawa amesema hayo alipotembelea kitongoji cha Kiembeni wilayani Bagamoyo ikiwa ni muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kutatua kero za maji. Prof. Mbarawa amewatoa wasiwasi wakazi wa wilaya hiyo na kuwataarifu Sh. 116 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha mradi mkubwa wa maji ambao utahudumia wilaya nzima ya Bagamoyo, Pwani kwa ujumla pamoja na jiji la Dar es salaam

Aidha, Waziri huyo amesema fedha za mradi huo zipo tayari na wanasubiri bodi kupitisha. Prof. Mbarawa pia amewaambia wananchi hauo kuwa wapo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo mkubwa wa maji katika wilaya ya Bagamoyo na kuwataka wakazi wa wilaya hiyo kutunza miundombinu pamoja na kuwataka kulipa bili za maji vizuri ili kuendelea kupata huduma bora ya maji.

“Tayari pesa ipo na lengo letu ifikapo 2020 tuwe tumefikisha asilimia 95 ya wananchi wanaopata huduma ya majisafi na salama, naomba niwahakikishie watanzania kwama watapata maji wote kwa sababu serikali imekuja na mpango wa kuchukua maji kutoka vyanzo vya maji na kuyafikisha sehemu ya makazi ya wananchi”. Ameelez Prof. Mbarawa.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter