Home BIASHARAUWEKEZAJI Watanzania watakiwa kuwa na uthubutu

Watanzania watakiwa kuwa na uthubutu

0 comment 159 views

Watanzania wametakiwa kuwa na uthubutu wa kufanya biashara na kuwekeza katika maeneo mbalimbali badala ya kutegemea watu kutoka nje ya nchi katika uwekezaji.

Ally Dahal, ambae ni Mkurugenzi wa Jochata Vocational Centre ametoa wito huo katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba jijini Dar es Salaam.

“Watanzania wengi hawana uthubutu wa kuanzisha biashara, wanakuwa na hofu ya kipato na wengine wanasubiri kuona mwingine akifanya ndipo na yeye aanze kufanya,” ameeleza Ally.

Wakiwa katika viwanja vya maonesho, Jochata ambao ni watengenezaji wa machine mbalimbali wameonesha mashine ya kuchakata plastiki, karatasi na vioo ambayo inatengenezwa hapa nchini.

“Katika haya maonesho tunaona muamko mkubwa wa watu mbalimbali wakitaka kujua jinsi mashine hii inavyofanya kazi, lakini wengi wanaonekana kutokuwa na uthubutu wa kujaribu.

Biashara ya plastiki ni kubwa ambapo kuna kampuni za China na Uturuki wananunua plastiki. Ukiwa na mashine hii ya kuchakata unaweza kuwauzia plastiki ambayo imekwisha chakatwa kwa takribani Tsh 800 kwa kilo moja tofauti na kuuza kopo kwa Tsh 300 kwa kilo, hii ni fursa ambayo imejificha” ameeleza.

Amewataka vijana kujituma na kuwa na uthubutu wa kutumia fursa zilizopo.

“Kazi ya kukusanya au kuokota chupa inaonekana ni kazi ya watu wa hovyo lakini ni sehemu ambayo mtu anaweza kuwekeza na kujipatia kipato,” amesema.

Ameeleza kuwa mashine hiyo ambayo inatumia umeme ni rahisi kutumia.

Moja ya mashine ya kuchakata ikiwa katika maonesho ya Sabasaba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter