Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji dawa za mifugo washauriwa kuchangamkia fursa

Wawekezaji dawa za mifugo washauriwa kuchangamkia fursa

0 comment 112 views

Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa za mifugo,ili kukidhi mahitaji na upatikanaji wa dawa hizo kwa uhakika. Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alipotembelea kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya wanyama Kanda ya Ziwa (ZVC) na wakala wa maabara na Mifugo (TVLA) jijini Mwanza.

“Kuna fursa kubwa ya kuwekeza kwenye viwanda vya dawa za mifugo,serikali inatengeneza mazingira na miundombinu mizuri kwa ajili ya uwekezaji,hivyo wadau wajitokeze “Alisema Ulega.

Tanzania ni nchi ya tatu barani Afrika kwa wingi wa mifugo, lakini kumekuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa dawa. Waziri Ulega ameeleza kuwa, Tanzania ina takribani ng’ombe milioni 30, mbuzi milioni 15, kondoo takribani milioni 8, nguruwe milioni 5 na kuku wapatao milioni 60.

Awali Kaimu Ofisa Mfawidhi ZVC, Dk Subira Mwakabumbe alisema kwa mwaka 2016/17 mikoa sita ya kanda ya ziwa katika halmashauri za Kahama, Missenyi, Biharamulo, Rorya na Ushetu ng’ombe 178 walikufa kutokana na homa ya mapafu,huku 56420 wakichinjwa kuzuia ugonjwa huo kuenea zaidi. Aidha, katika wilaya za Nyamagana, Ilemela (Mwanza) na Bukoba mkoani Kagera nguruwe 2430 waliripotiwa kufa kutokana na homa ya nguruwe.

Naye Meneja wa TVLA Dk. Joseph Genchwere amedai sampuli 5323 zimeshakusanywa huku changamoto kubwa ikiwa ni mwitikio mdogo wa wafugaji kupeleka sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara kubaini ugonjwa ili kutoa tiba.

Tanzania ni nchi ya Tatu barani Afrika kwa wingi wa mifugo lakini inakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa, tatizo ambalo linahitaji uwekezaji wa viwanda vya utengenezaji na uzalishajiwa dawa za mifugo ili kutatuliwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter