Home BIASHARA Wajasiriamali Singida kusafirisha asali nje

Wajasiriamali Singida kusafirisha asali nje

0 comment 121 views

 

Na Mwandishi wetu

Kundi la vijana wajasiriamali kutoka Singida wanategemea kuanza kusafirisha asali kwenda nchi za Ulaya na Ujerumani. Singida Youth Enterpreneurs and Consultants Cooperative Society (SYECCOS) wamekua katika mazungumzo na wateja kutoka nchi hizo. Mwezi ujao wawakilishi wa wajasiriamali hawa wanategemea kwenda kwenye kongamano la kimataifa nchini Turkey ambapo ndio wanategemea kufikia makubaliano.

Wateja hao kutoka nchi za Ulaya na Ujerumani wanategemea kuagiza karibu tani 50,000 za asali kila mwaka. Kutokana na uhitaji wa bidhaa hiyo, wajasiriamali hao wanaweza kuongeza kiwango cha mavuno yao. Takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa Wizara ya  Maliasili na Utalii huvuna  tani 34,000 na kusafirisha tani 500 kwa mwaka, wateja wakubwa wakiwa Ulaya,Uarabuni na Marekani.

Tangu mwaka 2013 vijana kutoka Singida wamekuwa wakitoa mafunzo na matokeo yanaonyesha kwamba wanunuaji kutoka Ujerumani na Turkey wameridhika na kiwango cha asali kutoka mkoani hapo. Mazungumzo ya kusafirisha asali ya Singida yalianza tangu 2013. SYECCOS pia watanunua asali kutoka kwa wafugaji wengine wa nyuki ili kuwa na uhakika wa kufikia tani 50,000 zitakazosafirishwa.

SYECCOS wamewekeza Sh 1.5 bilioni katika mradi huu. Miaka ya myuma miradi ya asali Tanzania haikufanya vema kutokana na uwekezaji wa chini lakini msemaji wa taasisi hii Bw. Philemon Kiemi amesema kwamba wana uhakika na ubora  ya asali hii kwani imefanyiwa majaribio nchi za nje.Ameongezea kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha mavuno yanaongezeka kutokana na mahitaji ya soko.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter