Home FEDHABIMA Faida nne za bima ya maisha.

Faida nne za bima ya maisha.

0 comment 133 views

Mara nyingi taasisi za bima zikihamasishwa wananchi kuwa na aina hii ya bima kama ilivyo kwa zile za kawaida kama bima ya gari, afya, moto. Jambo la muhimu ambalo kila mtu anatakiwa kujua ni kwamba siku zote ni kwamba kila bima ina umuhimu wake na kama upo katika nafasi ya kuwa nazo, ni vizuri kuchukua fursa hiyo kwa ajili ya manufaa ya baadae.

Bima ya maisha ni bima muhimu hasa kwa watu ambao wana familia na majukumu mbalimbali katika jamii kwa sababu jambo lolote likitokea, bima hii huwa na msaada mkubwa kwa familia.

Hizi hapa ni baadhi ya faida za kuwa na bima ya maisha.

Gharama za mazishi

Mara nyingi watu huwa wanakuwa hawajajiandaa kumzika mpendwa wao. Hivyo ili kuwaepushIa ndugu, jamaa na marafiki changamoto ya kutafuta fedha kwa ajili ya mazishi, kupitia bima ya maisha unaweza kuwaondolea changamoto hiyo kwani unakuwa na uhakika kuwa familia ndugu na jamaa watawezeshwa kumudu gharama hizi bila vikwazo vyovyote.

Kusaidia familia

Kila mzazi hufurahishwa zaidi pale watoto wakiwa na mahitaji yote kama vile ada za shule, mavazi na malazi. Ikiwa unataka maisha ya watoto wako kuendelea kama kawaida na kuondoa changamoto kuhusu masuala ya kifedha, kuna umuhimu mkubwa wa kujipatia bima ya maisha ili kuhakikisha maisha ya baadae ya watoto wako yatakuwa salama hata kama hautokuwepo.

Kulipa madeni

Mbali na kulipia gharama za maisha za kila siku, kupitia bima ya maisha ikiwa familia ina madeni basi wanaweza kulipa madeni hayo kupitia bima hiyo. Hii inasaidia kuepuka maamuzi magumu kama vile kuuza nyumba, samani nk kwa ajili ya kulipa fedha zinazodaiwa. Bima hii inawezesha maisha kuendelea bila ugumu ambao mara nyingi unatokana na madeni.

Upangaji wa biashara

Ikiwa unamiliki biashara ni muhimu kuwa na bima ya maisha ili kulinda biashara yako na ikitokea unashirikiana na mtu ni muhimu kwa wote kuwa na bima hii ili lolote litakalotokea lisiathiri mwenendo wa biashara katika masuala ya fedha. Pia washirika kuwa na bima huondoa usumbufu wa kuanza kutafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi yake.

Katika karne hii wazazi wanafanya kazi kwa bidii ili kuweza kupata kipato na kuhudumia familia. Hata kama mzazi mmoja ana kipato kikubwa kuliko mwingine ni vyema kwa wazazi wote kuwa na bima ya maisha ili hata mmoja wao akiondoka, basi mwenendo wa maisha unaendelea kama kawaida.

Gharama za bima ya maisha hutegemea na muda. Kuna bima za maisha kwa muda wa miaka 10, 20, 30 n.k.  Ni muhimu kufanya maamuzi kwanza kutokana na kiasi unachoweza kumudu. Pia angalia ni mambo gani yanaweza kubadilika kisha fanya maamuzi ili kuhakikisha maisha ya wapendwa wako yatakuwa salama bila wewe.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter