Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Vidokezo muhimu vya fedha kwa vijana

Vidokezo muhimu vya fedha kwa vijana

0 comment 230 views

Kwa bahati mbaya elimu kuhusu fedha binafsi huwa haitolewi katika shule na vyuo vingi. Kutokana na hilo vijana wengi hukosa elimu ya msingi  kuhusu fedha hivyo kuwafanya wakose matumaini kuhusu jinsi ya kudhibiti fedha zao, kuomba mikopo, na vilevile kujiepusha na madeni.

Kama kijana, ili kuelewa zaidi masuala ya fedha na kuishi maisha mazuri yenye mafanikio ni muhimu kujua vidokezo vifuatavyo;

Jifunze kujizuia

Kuna baadhi ya vijana ambao wamebahatika kufundishwa na wazazi wao kuhusu kujizuia walipokuwa watoto. Hivyo kama hukufundishwa ni muhimu kujua kadri utakavyowahi kujifunza kujizuia ndivyo mabadiliko yatakavyotokea katika masuala yako ya kifedha. Hivyo jenga tabia ya kulipa fedha taslimu kwa vitu unavyohitaji/vya muhimu. Pia epuka kukopa ikiwa huna sababu maalum.

Dhibiti mustakabali wako wa kifedha

Ikiwa hutajifunza kusimamia fedha zako mwenyewe, watu wengine watatafuta njia ya kusimamia fedha zako. Baadhi ya watu hao wanaweza kuwa na nia mbaya, na wengine wanaweza kuwa na nia nzuri lakini watakuwa wanajua mapungufu yako. Badala ya kutegemea ushauri kutoka kwa watu wengine, chukua hatua na anza kwa kujisomea vitabu kuhusu masuala ya fedha binafsi. Siku zote kuelewa fedha zinavyofanya kazi huwa ni hatua ya kwanza ya kuzifanya fedha hizo zikufanyie kazi. Ikiwa unataka maisha yako ya baadae yawe mazuri basi ni muhimu kujua fedha zinavyofanya kazi na sehemu ya kuziweka ili ziweze kuzalisha faida.

Jua fedha zako zinakwenda wapi

Baada ya kupata elimu ya msingi kuhusu masuala ya fedha binafsi, ni dhahili kuwa utaona kuwa kuna umuhimu wa gharama za matumizi yako kutokuzidi mapato yako. Na njia bora ya kuwezesha hilo kufanyika ni kuweka au kutengeneza bajeti. Pia hakikisha gharama zako za mwezi zipo chini. Ikiwa hutopoteza fedha zako kukaa katika ghorofa la kifahari sasa unaweza kumiliki nyumba nzuri zaidi muda si mrefu kwa sababu ya bajeti.

Anzisha mfuko wa dharura

Moja ya mambo ambayo hurudiwa kila siku ni pamoja na “kujilipa kwanza” bila kujali una madeni kiasi gani, au una mshahara mdogo kiasi gani. Ni muhimu kutafuta kiasi chochote katika bajeti yako na kukiweka katika mfuko wa dharula kila mwezi.

Anza kuweka akiba

Ni muhimu kwa kila kijana kufikiria maisha baada ya kustaafu. Hivyo kwa kuanza mapema kuweka akiba, kutakusaidia kuwekeza na kuweza kupata fedha kwa ajili ya maisha baada ya kustaafu. Kuna baadhi ya kampuni hufadhili mipango ya kustaafu mara nyingi mipango hiyo huwa na mikakati rafiki kwa wafanyakazi hivyo sio vibaya kujiunga nayo.

Kuwa na uelewa wa masuala ya kodi

Hata kabla hujapata mshahara wako wa kwanza ni muhimu kujua mambo kadhaa kuhusu kodi. Wakati kampuni inakupa mshahara, unahitaji kujua jinsi ya kuhesabu ikiwa mshahara huo utakupa fedha za kutosha baada ya kodi kufikia malengo. Bahati nzuri siku hizi unaweza kufanya mahesabu hayo kupitia mtandao na kujua kiasi gani kinakwenda katika kodi.

Linda afya yako

Ikiwa kufikia malipo ya bima kwa mwezi ni jambo lisilowezekana, Je utafanyaje ikiwa unatakiwa kwenda katika chumba cha dharura kwa sababu ya magonjwa ambayo hukupanga kupata? Kama huna bima ya afya ni muhimu kuipata ili kuweza kurahisisha gharama ikiwa ajali au magonjwa yatakupata. Unaweza kujipatia bima ya afya kwa bei nafuu kutoka NHIF.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter