Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Vijana na biashara ya kuku choma Dar

Vijana na biashara ya kuku choma Dar

0 comment 510 views

Ukipita maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam hasa nyakati za usiku, utawaona vijana wakifanya biashara ya kuuza kuku choma kandokando mwa barabara.

Biashara hii imeshamiri na imewasaidia vijana wengi kujiajiri na kujipatia kipato.

Watu wengi wanapotoka makazini na kwenye pilika pilika za kila siku, hupitia kitoweo hicho cha kuku choma kwa ajili ya mlo.

Wengine husimama na kula hapo hapo huku wengine wakiagiza kufungiwa (take away) na kwenda nacho nyumbani kula na familia.

Kitoweo hicho, kimeonekana kuwa rahisi kutokana na bei yake pamoja na kuwa kipo tayari kwa kula, yaani kimeshaandaliwa na kuchomwa vizuri.

Kuku hao huuzwa kati ya Sh 2000 na Sh 2500 kwa kipande.

Idi ni kijana anaefanya biashara ya kuuza kuku choma eneo la Kimara, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Anasema biashara hiyo inamsaidia kumpatia kipato na kuendesha maisha yake.

“Kwa kweli japo hali ni ngumu lakini biashara hii ya kuuza kuku wa kuchoma inanisaidia, napa faida na ndio maana hadi sasa naifanya.” Amesema Idi.

Ameeleza kuwa kwa siku anachoma kuku hadi 80 huku akibainisha kuwa anapata faida ya Sh 1000 kwa kila kuku.

“Faida inapatikana Sh 1,000 kwenye kila kuku, na faida yenyewe inatokana na firigisi na shingo. Ingawaje faida sio kubwa lakini sio sawa na bure.” Amesema.

Akizungumzia swala la changamoto Idi anasema “changamoto kubwa ni karatasi za kufungashia chakula (Foil paper) ambapo bei yake imekuwa ikiongezeka siku hadi siku. Tulikuwa tunanunua Sh 10,000 lakini sasa hivi tunanunua hadi Sh 14,000”.

Mmoja wa wateja wa Idi aliejitambulishwa kwa jina la Irene anasema anapenda kitoweo hicho kwani mbali na kuwa na ladha nzuri, pia hurahisisha mlo wake wa usiku.

“Nikitoka kazini napitia hapa nauua kipande cha kuku japo sio kila siku, naaweza kula na ugali ama ndizi za kukaaga, na wakati mwinginne akula kipade hicho a matunda nalala, yaani haawa kuku wamerahisisha sana suala la mapishi maana wakati mwingine unakuwa umechoka na kazi.” ameeleza.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter