Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI SIDO kuchochea uchumi wa viwanda

SIDO kuchochea uchumi wa viwanda

0 comment 119 views

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji amesema shirika hilo kwa kushirikiana na mkoa wa Simiyu wameandaa maonyesho ya kitaifa ya wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuhamasisha jamii kujenga na kuanzisha viwanda vidogo. Prof. Mpanduji amesema maonyesho hayo yatafanyika mkoani Simiyu kuanzia tarehe 23 hadi 28 mwezi Oktoba na mbali na uhamasishaji, pia yataonyesha teknolojia za kisasa za uzalishaji.

“Haya ni maonyesho ya kwanza ya kitaifa kwa wajasiriamali ambayo yanashirikisha pia taasisi za kifedha, taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo TBS, TDF na wengine ili kusaidia kutoa muongozo katika uzalishaji”. Amesema Prof. Mpanduji.

Mbali na hayo, Mkurugenzi huyo pia amedai kuwa maonyesho hayo ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali kuonyesha ubora wa bidhaa zao kwani ni nafasi mojawapo ya kutafuta masoko ya uhakika na kujitangaza.

“Maonyesho haya ya kitaifa yatakuwa yakifanyika kila mwaka katika mikoa mbalimbali. Mwaka huu tunaanza na mkoa wa Simiyu”. Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Pamoja na kuwataka wadau mbalimbali kuchangamkia maonyesho hayo, Prof. Mpanduji pia amesema wamealika washiriki kutoka mataifa ya India, China na Ujerumani ili kuongeza motisha na kutambulisha teknolojia mpya za uzalishaji wa viwandani.

“Tumejipanga kufanikisha azma ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025”. Amesisitiza Prof. Mpanduji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter