Na Mwandishi wetu
Viongozi wilayani Kyerwa mkoani Kagera wamepiga marufuku biashara ya kahawa changa na kuwataka wakulima wauze kahawa yenye viwango vinavyotakiwa sokoni ili wafaidike na kilimo hicho.
Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Shaabani Lissu amewaambia waandishi wa habari kuwa, biashara ya kahawa changa maarufu kama obutura haiwaondoi wakulima katika hali ya umaskini. Amewataka maofisa ugani kutoa elimu kwa wakulima ili wabadilike.
Baadhi ya wakulima katika wilaya hiyo wamesema sababu zinazopelekea wao kufanya biashara ya kahawa changa ni wao kukosa fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya familia zao na pia ukosefu wa elimu.