Home KILIMOKILIMO BIASHARA Bodi ya mkonge yatakiwa kufanya utafiti wa masoko

Bodi ya mkonge yatakiwa kufanya utafiti wa masoko

0 comment 249 views

Naibu Katibu Mkuu – Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji), Dkt. Suleiman Serera, ameitaka Bodi ya Mkonge kufanya utafiti wa masoko kwa ngazi ya kimataifa ili kujua hali ya bei ya Mkonge ikilinganishwa na hapa nchini.

Ameyasema hayo Novemba 18, 2024 wakati alipofanya kikao na Viongozi wa Bodi ya Mkonge na Wadau wa Kilimo wakati wa ziara ya kutembelea Vyama vya Ushirika , Skimu za Umwagiliaji na Miradi ya Maendeleo Jijini Tanga.

“Tujifunze kwa nchi za wenzetu, tuone ni kwa namna gani wanavyoweza kufanya uzalishaji na kujua ni viwanda vya aina gani tunatakiwa kuwa navyo kwakuwa kupitia kujifunza ndipo tunakoweza kupata fursa na mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya masoko ya zao la mkonge,” amesema Dkt. Serera.

Naibu Katibu Mkuu – Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji), Dkt. Suleiman Serera, akionesha bidhaa itokanayo na mkonge.

Aidha, Dkt. Serera ameitaka Bodi ya Mkonge kutafuta fursa ya uzalishaji wa mkonge katika mikoa mingine ili kuongeza uzalishaji na kukuza pato la taifa.

Naibu Katibu Mkuu – Kilimo ametoa rai kwa Wakulima wa zao la Mkonge kujifunza na kuona faida za Ushirika kwa kujiunga na AMCOS ambazo zinawasaidia wakulima kuwa pamoja na hata kujiunga na SACCOS ambazo ni suluhisho la mtaji.

Katika ziara hiyo Dkt. Serera alipata nafasi ya kutembelea Chama Kikuu cha Ushirika cha Maziwa cha mkoa wa Tanga (TDCU) na kufanya mazungumzo na viongozi wa Bodi ya Chama na kujadili mafanikio na changamoto za Chama hicho.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter