Home KILIMOKILIMO UFUNDI Tanzania, Ujerumani kubadilishana teknolojia sekta ya kilimo

Tanzania, Ujerumani kubadilishana teknolojia sekta ya kilimo

0 comment 67 views

Serikali ya Ujerumani imesema ipo tayari kubadilishana teknolojia za kisasa na mifumo bora ya Kilimo wanayotumia itakayowawezesha wakulima wa Tanzania kuinua kiwango cha uzalishaji mazao mbalimbali ili iweze kuzalisha mazao hayo na yaweze kupata soko katika Bara la Ulaya.

Hayo yameelezwa katika kikao kazi kati ya Tanzania na Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Bavaria, nchini Ujerumani.

Tobias Gotthardt Naibu Waziri wa Uchumi, Maendeleo ya Kikanda na Nishati wa Jimbo la Bavaria, Ujerumani aliongoza ujumbe huo ambapo amesema nchi hiyo ipo tayari kubadilishana teknolojia za kisasa ili kuinua kilimo Tanzania.

Tobias Gotthardt Naibu Waziri wa Uchumi, Maendeleo ya Kikanda na Nishati wa Jimbo la Bavaria, akizungumza katika kikao kazi baina ya Tanzania na Ujerumani.

Kwa upande wa Tanzania kikao hicho kiliongozwa na Dk. Hussein M. Omar, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo kilichofanyika Novemba 01, 2024 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine viongozi hao walijadiliana kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Bavaria. Wakati wa majadiliano, Dk. Hussein alieleeza kuhusiana jitihada mbalimbali zinazofanyika na Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha Sekta ya Kilimo ikiwemo, kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali, kuimarisha miundombimu ya umwagiliaji, kuongeza upatikanaji wa pembejeo za kilimo na Sekta ta kilimo inavyochangia katika upatiakanaji wa ajira kwa vijana kupitia Programu ya Jenga Kesho Bora (BBT-YIA).

Aidha, alieleza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Bavaria katika maeneo mbalimbali ya ambapo alieleza kuwa Tanzania na Bavaria zinaweza kushirikiana katika kuimairisha utafiti katika kilimo kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mbegu bora zinazostahmili ukame, teknolojia za uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Nyingine ni kushirikiana katika katika kuongeza upatikanaji wa masoko ya mazao na eneo la uongezaji thamani wa mazao na teknolojia za kuhifadhi mazao ya wakulima.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Hassan Iddi Mwamweta, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani pamoja na viongozi na Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter