Home KILIMO Muhogo kupata soko la uhakika China

Muhogo kupata soko la uhakika China

0 comment 95 views

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Siza Tumbo ametoa wito kwa wadau wa zao la muhugo hapa nchini kuongeza uzalishaji kwani serikali ipo tayari kuwawezesha kupata soko la uhakika nchini China. Prof. Tumbo ametoa ushauri huo kwenye mkutano wa wadau wa zao hilo kitaifa ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA), Wizara ya Kilimo, Kitengo cha Mpango wa Maendeleo ya sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Katika maelezo yake, Naibu Katibu huyo ameeleza kuwa hatua hiyo itapelekea taifa kuongeza wigo wa kusafirisha mihogo China ambapo kwa mwaka 2017, inakadiriwa kupeleka bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani laki tatu (Sh. 687 milioni), huku China ikiingiza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.1 hapa nchini.

“Uzalishaji upo chini kitakwimu lakini kiuhalisia haipo hivyo, sasa tunatakiwa tuwe ma champion kwenye uzalishaji wa zao hili ni zuri sana ili tuweze kuleta mageuzi kwenye zao hili”. Amesema Prof. Tumbo.

Tanzania ni nchi ya kumi na mbili kwa uzalishaji wa muhogo duniani na ya sita barani Afrika baada ya Nigeria, DRC, Ghana, Angola na Msumbiji ambapo kila mwaka, unachangia asilimia 5.5 ya jumla ya uzalishaji wake duniani na asilimia 14 kwa Afrika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter