Home KILIMO Wakulima wa mpunga washauriwa kuunda ushirika

Wakulima wa mpunga washauriwa kuunda ushirika

0 comment 115 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakulima wa zao la mpunga kutoka Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuanzisha Chama cha Ushirika kwa ajili ya zao hilo ili wauze kwa bei wanayotaka. Majaliwa amedai wakulima hasa wa mazao ya chakula na biashara wamekuwa wakitumia nguvu na fedha nyingi katika uzalishaji lakini kutokana na kila mmoja kuuza kwa bei yake, wamekuwa wakipata fedha kidogo.

Majaliwa amedai serikali inadhamiria kuona wakulima wote hapa nchini wakinufaika na kilimo chao na kuagiza kaofisa kilimo kuwatembelea wakulima mashambani katika maeneo yao na kuwaelimisha kuhusu namna ya kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija.

Pamoja na yote hayo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wakulima kujenga mazoea ya kutunza fedha wanazopata baada ya kuuza mazao ili ziwasaidie kujiandaa na msimu unaofuata na pia kuondokana na madeni kwani wengi hukopa fedha na kuzitumia katika shughuli za kilimo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter