Home KILIMO Wakulima walalamikia bei ya pamba

Wakulima walalamikia bei ya pamba

0 comment 106 views

Wakulima wa pamba mkoani Geita wameiomba serikali kuangalia namna ya kuwasaidia ili kuhakikisha bei ya zao hilo inawanufaisha wakulima. Mbali na changamoto ya bei, wakulima hao wametoa wito kwa serikali kutoa viuatilifu vya kutosha ili waweze kuzalisha mazao bora na yenye tija.

Soma Pia Kero hizi zitatuliwe kuinua kilimo

Akizungumza katika kikao  kilichowakutanisha viongozi wa serikali za vijiji na kata, maofisa kiimo na wananchi, mmoja ya wadau wa zao hilo amedai mkulima mwenye heka 10 amekuwa akipatiwa chupa moja ya viuatilifu, kiasi ambacho hakitoshelezi na inakatisha tamaa kwa wakulima hao kuendelea kuweka nguvu katika uzalishaji wao.

Akitolea ufafanuzi kuhusu kero hiyo, Afisa Kilimo kata ya Butizya, Rhoda Mbonye amesema kuwa wakulima wengi wanakata tamaa kutokana na kutorejesha gharama za uzalishaji wanapouza mazao yao na hivyo kupata hasara. Naye Joseph Machibya ambaye ni Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Bukombe, amedai serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba nchini ndiyo wamekuwa wakipanga bei ya zao hilo kwa kuangalia bei ya soko la dunia.

Soma Pia Wasomi washauriwa kuchangamkia kilimo

Kuhusu uhaba wa viuatilifu, Machibya amesema wakulima wapatao 13,569 ndio waliofaidika na viuatilifu kupitia usajili uliofanyika katika vijiji mbalimbali ikiwa ni matokeo ya udhamini kutoka kampuni za ununuzi wa pamba. Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amewataka viongozi wa kata na vijiji kufuatilia wananchi wote wanaodaiwa na serikali huku akionya kuwa, watakaokiuka watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter