Home Uncategorized Hii hapa Huawei Mate 30 Pro

Hii hapa Huawei Mate 30 Pro

0 comment 129 views

Licha ya kuwepo kwa migogoro ya kibiashara baina ya serikali ya China na Marekani, kampuni ya Huawei imezindua rasmi toleo jipya la simu za Huawei Mate 30 na Mate Pro Septemba 19 mwaka huu. Baadhi ya mambo makubwa ambayo yamekuwa ni gumzo kuhusu simu hizo ni maboresho makubwa ya kamera pamoja na kukosekana kwa programu zilizopo chini ya kampuni ya Google zikiwemo Google Playstore, Google Maps na Google Chrome.

Simu hizo zinakuja na mfumo mpya unaofahamika kama Huawei Mobile Services (HMS) badala ya Google Mobile Services (GMS) ambayo ilikua inaruhusu matumizi ya teknolojia za mawasiliano zilizopo katika simu ikiwa ni pamoja na programu. Kutokana na mabadiliko hayo, simu hizi mpya zina programu 45,000 pekee ikilinganishwa na programu milioni 2.7 zilizopo Google Playstore.

Hizi hapa ni baadhi ya sifa za Huawei Mate 30 Pro

Simu ya Huawei Mate 30 Pro ina kioo cha ukubwa wa inchi 6.53 chenye teknolojia ya OLED capacitive touchscreen ambacho kina uwezo wa kuonyesha rangi milioni 16.

Mfumo wa uendeshaji katika simu hii ni Android 10 yenye mfumo wa Huawei EMUI 10. Uwezo wa Processor katika simu hii ni Octa-core (2×2.86 GHz Cortex-A76 & 2×2.09 GHz Cortex-A76 & 4×1.86 GHz Cortex-A55).

Uwezo wa GPU ni Mali G76 MP 16 huku aina ya Processor (Chipset) ni HiSilicon Kirin 990 yenye mfumo wa 5G. Ukubwa wa ndani (Internal Memory) ni GB 128 ambayo inaweza kuongezeka na Nanocard ya GB 256. Katika aina zote mbili zinakuja na RAM ya GB 8

Katika upande wa kamera; ya mbele inakuja na uwezo wa Megapixel 32 yenye lensi ya Leica. Kamera ya nyuma inakuja na kamera nne ambazo zina uwezo wa Megapixel 40 (wide angle),  Megapixel 8 (telephoto) na Megapixel 40 (Ultra wide angle) na kamera nyingine ya video yenye 3D TOF. Kamera zote zinakuja na uwezo wa kuchukua video hadi za 4K, pia kuna portrait mode na night mode.

Katika upande wa betri kuna betri isiyotoka ya Li-Po 4500 mAh ambayo ina uwezo wa kuchaji haraka (Fast charging), kuchaji bila waya (wireless charging pamoja na reverse wireless charging) .

Simu ya Huawei Mate 30 Pro inakuja na rangi sita ambazo ni Space Silver, Emerald Green, Cosmic Purple, Black, Vegan Forest Green, Vegan Orange.

Pia katika simu hii kuna sehemu ya ulinzi ya Fingerprint pamoja na sensa maalumu ambazo zinaweza kutambua uso na macho yako na uwezo wa kuzuia maji kuingia katika simu (water resistant). Aidha mtumiaji anaweza kutumia mfumo wa 2G, 3G, 4G hadi 5G.

Gharama ya simu hiyo inategemea mfumo wa 5G. Wale watakaonunua simu hiyo bila mfumo huo mpya wa 5G watalipia Euro 1,100 ambayo ni takribani Sh. 2,782,293.70 kwa fedha za Tanzania, huku wale watakaonunua simu hiyo pamoja na mfumo huo wa 5G watalipa Euro 1,200 ambayo ni sawa na Sh. 3,035,229.49.

Je, unaizungumziaje simu hii mpya kabisa ya Huawei?

 

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter