Kampuni ya ufuaji umeme kwa kutumia gesi, Songas imetoa vifaa vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 katika wilaya ya Ubungo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Kisa Makori, Meneja Uhusiano wa Songas Bw. Nicodemus Chipakapaka alisema vifaa hivyo ni mpango wa Songas kutia nguvu katika juhudi za serikali za kuhifadhi na kutunza mazingira hasa katika kipindi hiki ambacho dunia imesheherekea wiki ya mazingira.

Meneja uhusiano wa jamii wa Kampuni ya nishati, Songas, Bw Nicodemus Chipakapaka (kushoto) akizungumza katika hafla ya ukabidhi wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Kisa Makori katika viwanja vya Manzese Bakhresa jijini Dar es Salaam wikiendi. Vifaa hivyo ni sehemu ya mchango wa Kampuni ya Songas ili kutia nguvu mpango wa serikali wa kutunza na kuhifadhi mazingira, hasa hasa tukielekea maadhimisho ya wiki ya mazingira inayosherekewa duniani kote kila tarehe 6 Juni.

Meneja Uhusiano wa Jamii Kampuni ya Songas, Nicodemus Chipakapaka (kulia) akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Ubungo, Kisa Makori (Kushoto) vifaa vya usafi vyenye thamani ya Shilingi milioni 10 katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Manzese Bakhresa jijini Dar es Salaam, jana. Vifaa hivyo ni sehemu ya mchango wa Kampuni ya Songas ili kutia nguvu mpango wa serikali wa kutunza na kuhifadhi mazingira, hasa hasa tukielekea maadhimisho ya wiki ya mazingira inayosherekewa duniani kote kila tarehe 6 Juni.