Home VIWANDA Takataka kutumika kama malighafi Kinondoni

Takataka kutumika kama malighafi Kinondoni

0 comment 68 views

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema mradi wa ujenzi wa kiwanda cha mbolea ambacho kitatumia malighafi ya takataka unatarajiwa kuanza Septemba mwaka huu baada ya taratibu zote kukamilika.

Mradi huo kwa mujibu wa Meya Sitta utagharimu zaidi ya Sh. 4 bilioni na unafadhiliwa na jiji la Hamburg la nchini Ujerumani. Sitta pia ameeleza kuwa manispaa ya Kinondoni ipo katika hatua za mwisho za kutafuta mkandarasi atakayeshughulikia ujenzi wa kiwanda hicho katika eneo la Mabwepande.

Manispaa inatakiwa kutenga eneo la ujenzi huo na pia kugharamia miundombinu ya barabara, umeme na maji ambayo Sitta amesema watatekeleza. Ameongeza kuwa mradi huu ukikamilika utaongeza mapato ya manispaa hiyo na pia utapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya taka katika masoko yaliyopo katika manispaa hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter