Home VIWANDA Ajenda ya viwanda 100 yawabana wakuu wa mikoa

Ajenda ya viwanda 100 yawabana wakuu wa mikoa

0 comment 102 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza wakuu wa mikoa yote kutoa taarifa za kila robo mwaka za maendeleo ajenda ya viwanda 100 ili kusaidia kutambua taifa lilipofikia katika utekelezaji wa malengo ya uchumi wa kilimo na viwanda ifikapo mwaka 2025. Waziri Majaliwa amesema hayo katika kongamano la kitaifa la baraza la uwezeshaji kiuchumi ambapo amedai kuwa, taarifa zitakazopatikana zitatumika kama kipimo cha uwajibikaji kwa wakuu wa mikoa katika utekelezaji wa malengo yaliyopo kuinua uchumi wa taifa.

Kongamano hilo la tatu linawakutanisha wadau wanaotekeleza sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kupata mrejesho wa uchumi na changamoto zake katika kila mwaka.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa baraza la taifa la uwezeshaji kiuchumi Dk. John Jingu amesema viwanda ni nyenzo dhabiti ya kupambana na umaskini na kuboresha maisha ya wananchi.

Naye Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ametoa wito kwa taasisi za fedha kuanza kuwaamini wawekezaji wa ndani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter