Home VIWANDA JPM azindua kiwanda cha mahindi Ruvuma

JPM azindua kiwanda cha mahindi Ruvuma

0 comment 97 views

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amezindua kiwanda cha kuchakata mahindi kilichojengwa kwa thamani ya Sh. 444.77 milioni na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale, mkoani Ruvuma. Wakati wa uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema kuwa muda umefika kwa viwanda ambavyo vimebinafsishwa lakini havijaendelezwa kurudishwa serikalini pasipo kujali vinamilikiwa na nani.

“Hata kama waliovichukua walikuwa mawaziri shughulikieni suala la kuwanyang’anya. Wakitaka wapeleke mahakamani na mnaweza kuwapeleka kwa kuwashtaki kwa uhujumu uchumi. Wamechelewesha ajira za watanzania na mapato mara 10 wanaposhindwa huko, wapeni hawa ambao wanajua kuvitumia ili vijana wetu wapate ajira”. Ameeleza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli ametoa shukrani zake kwa JKT, baada ya kutoa gawio la Shilingi milioni 700 kwa mara ya kwanza na kusema fedha hizo zitasaidia katika kutekeleza bajeti ya nchi na kutoa wito kwa mashirika mengine kuiga mfano huo.

“Ikiwa JKT wametoa gawio mliobaki, kama wanajeshi wametoa gawio halafu mashirika mengine mtaji ni wa serikali, watendaji wakuu mmekaa tu, kamani mguu upande mguu sawa au mwili legeza sasa muanze”. Amesema.

Mbali na hayo, JPM pia amezitaka Kamati za Bunge kufuatilia mashirika ambayo hayatoi gawio wakati wahusika wanalipana mishahara mikubwa.

“Mtoe mapendekezo ndani ya serikali ili wahusika wote wakiwemo watendaji wakuu na bodi zao watupishe. Lazima ifike mahali tuelezane ukweli ili fedha hizi zijenge taifa”. Amesema.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter