Home VIWANDA Kongamano uwezeshaji kufanyika Juni 15

Kongamano uwezeshaji kufanyika Juni 15

0 comment 117 views

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bengi Issa amesema Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika kongamano la nne la kitaifa la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi litakalofanyika Juni 15 mwaka huu.

“Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi katika kongamano hili na atazindua ripoti ya mwaka ya uwezeshaji wananchi kuwatambua wadau wa uwezeshaji waliofanya vizuri kutoka kwenye wizara, idara, taasisi za umma na sekta binafsi kwa kuwapa tuzo na vikombe na vyeti”. Ameeleza Katibu huyo.

Pamoja na hayo, ameongeza kuwa kongamano hilo lenye kaulimbiu ya ‘Wezesha Watanzania kujenga Viwanda’ linalenga kujadili namna ya kufikia katika uchumi wa viwanda.

“Kama kaulimbiu inavyojieleza, tumeweka ujumbe huo kwa sababu tunaamini kuwezesha wananchi kujenga viwanda vitakavyotoa ajira nyingi, vitakavyowezesha wakulima kuzalisha mazao mengi na kuacha kuuza malighafi nje ya nchi”. Amesema.

Aidha, kupitia kongamano hilo, Issa ameeleza kuwa mada mbalimbali zitaibuliwa na wadau ili kupeana uzoefu katika masuala ya uwezeshaji kwa wananchi hususani mambo yanayohusu viwanda huku akitoa wito kwa wadau wa uwezeshaji kuhudhuria kongamano hilo ili kuweza kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter