Home VIWANDA Magufuli azindua kiwanda Rungwe

Magufuli azindua kiwanda Rungwe

0 comment 109 views

Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amezindua kiwanda cha maparachichi cha Rungwe Avocado Company Limited (RACL) eneo la Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Katika uzinduzi huo, Rais Magufuli ametoa pongezi kwa wamiliki kwa kutoa ajira kwa watanzania na vilevile kuwainua wakulima waishio maeneo ya jirani kwa kununua zao hilo.

Pamoja na kuwapongeza wamiliki hao, Rais Magufuli pia amewataka kutoa bei rafiki kwa wakulima ili waweze kunufaika na kilimo wanachofanya.

“Wakati serikali inashughulikia matatizo yenu na nyie toeni bei nzuri kwa wakulima na wafanyakazi wenu muwape mshahara mzuri ili waweze kufanya vitu vyao vizuri”. Amesisitiza JPM.

Kuhusu suala la kurejeshwa kwa VAT kwa wafanyabiashara pamoja na wawekezaji, Rais amesema mfumo huo umekuwa na changamoto kutokana na vitendo vya watu hao kuongeza gharama kwenye vitu ambavyo wanunua ili wapate fedha nyingi zaidi kutoka serikalini.

“Kulikuwa kukifanyika ‘Vat Refund’ hewa mtu amenunua vifaa vya Sh. 5 milioni anasema alinunua Sh. 50 milioni, tumelaliwa sana katika kipindi cha nyuma ndiyo maana serikali kupitia Wizara ya Fedha ikasema lazima ikague ‘Vat Refund’ zote kabla ya kufanyika malipo kama wanavyofanya katika nchi nyingine kabla ya kulipa lazima wathibitishe uhalali wa pesa mnazodai. Ninawahakikishia mtalipwa, ila mlete madai halali msiongeze na ikiwezekana mpunguze”. Amesema Rais Magufuli.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter