Home VIWANDAMIUNDOMBINU Bilioni 50 kukarabati uwanja wa ndege Mtwara

Bilioni 50 kukarabati uwanja wa ndege Mtwara

0 comment 95 views

Ofisa Uendeshaji wa uwanja wa ndege wa Mtwara, Zitta Majinge amesema serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imetenga Sh. 50 bilioni ili kukarabati uwanja huo na kurahisisha huduma za usafiri wa anga. Akizungumza na waandishi wa habari, Majinge amesema kuwa, karabati huo unahusisha ujenzi wa barabara ya urefu wa kilomita 1.2, maegesho ya ndege na njia za kuruka na kutua ndege. Akizungumzia ukarabati huo, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema unafanywa na Kampuni ya Beijing Constraction Engineering Group (BCEG) na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 2020.

“Ukarabati huo unafanywa na kampuni ya Beijing Constraction Engineering Group (BCEG) kwa muda ya miezi 24. Mkandarasi yupo katika hatua za maandalizi na ujenzi wa kambi ya Ofisi ya Mhandisi Mshauri”. Amesema Byakanwa.

Katika maelezo yake, Majinge, amesema urefu wa njia ya kuruka na kutua ndege hivi sasa ni mita 2,258 huku ndege zenye uwezo wa kutua uwanjani hapo kwa sasa ni zile zenye uzito wa tani 70. Imeelezwa kuwa baada ya ukarabati huo wanatarajia ndege zenye uzito wa tani 300 zitakuwa na uwezo wa kutua.

“Ukarabati ukikamilika kiwanja kitakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa zaidi. Hivi sasa makampuni mengi yanaomba kuja lakini yanashindwa kutokana na miundombinu mingi kuchoka hasa njia za kurukia na kutua ndege”. Amesema Majinge.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter