Home VIWANDAMIUNDOMBINU Msamaha wa kodi miradi ya maendeleo waanza rasmi

Msamaha wa kodi miradi ya maendeleo waanza rasmi

0 comment 106 views

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema serikali imeanza rasmi mchakato wa kutoa misamaha ya kodi kwa mikataba ya ujenzi na matengenezo ya miradi ya maendeleo ikiwemo viwanja vya ndege, barabara na madaraja ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Waziri Kamwelwe amesema hayo Manyoni mkoani Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akikagua hatua za ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station). Waziri huyo amedai sababu ya mradi huo kuchukua muda mrefu kukamilika ni mkandarasi kutopata msamaha wa kodi kama ilivyopangwa, jambo lililoathiri mtiririko wa fedha katika utekelezaji wake.

“Serikali imeanza kutekeleza misamaha ya kodi iliyokwama katika miradi inayoendelea na inayotarajiwa kuanza nchini, ikiwemo huu mradi na mingine mingi”. Amesema Mhandisi Kamwelwe.

Aidha, Waziri huyo ameagiza mkandarasi anayejenga kituo hicho, kampuni ya Impresa di Construction Ing E. Mantovani S.p. A con socio unico Via Belgio kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda alioomba kuongezewa na sio vinginevyo.

“Nahitaji kituo hiki kikamilike ifikapo Februari mwakani, kwani haya ni maazimio ya pamoja ya nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kupunguza ucheleweshwaji wa usafirishaji wa mizigo kupitia barabara ya kati kuelekea nchi jirani”. Amefafanua Waziri Kamwelwe.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter