Home VIWANDAMIUNDOMBINU Serikali kurasimisha makazi holela

Serikali kurasimisha makazi holela

0 comment 106 views

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuanzia sasa serikali haitabomoa nyumba za wananchi waliojenga maeneo yasiyo rasmi na badala yake, itarasimisha makazi holela na kuwapatia wananchi katika maeneo hayo hati rasmi. Waziri Lukuvi ameeleza hayo akiwa ziarani Simanjiro mkoani Manyara na kutoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Rais Magufuli.

“Serikali ya awamu ya tano inajali sana wananchi wake kwakuwa zamani wananchi ambao hawakujenga kwa kufuata mipango miji wangebomolewa nyumba zao, lakini kwa sasa serikali ya awamu ya tano imeanzisha mpango wa kurasimisha makazi holela na kuwapatia hati wananchi wote waishio mijini ili waishi katika makazi rasmi”. Amesema Lukuvi.

Pamoja na hayo, Lukuvi amewataka wananchi waishio mijini kurasimisha maeneo yao na kupata hati ili kulipa kodi ya pango la ardhi na kuchangia mapato serikalini.

“Nyumba isiyokuwa na hati haina thamani kwa kuwa hata ukienda benki kukopa pesa hawatakuuliza umejenga nyumba ya uzuri gani, lakini watakachotaka ni hati yako ya kumiliki ardhi ambacho ndio kitu kilicho na thamani zaidi kwako kuwa nacho”. Amefafanua Waziri huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter