Mawaziri na Makatibu wakuu kutoka wizara 14 zinazotekeleza mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler’s Gorge wamaeeleza kuridhishwa na kasi ya mradi huo. Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ta TANESCO Mhandisi Elangwa Abubakar amesema hivi sasa kazi ya ujenzi inaendelea na kwasababu ya ukubwa wa mradi huo, nguzo za zege zaidi ya 700 zitatumika kwa mara ya kwanza.
“Tunaendelea na ujenzi huku tukiwa tumezingatia masharti ya kitaalamu, ikiwemo kukata miti bila kuathiri mazingira kutoka usawa wa ndege. Kwa sasa kazi inayoendelea mafundi wanalaza kebo ambayo itazunguka na kupita chini ya reli na daraja. Awamu ya pili itakuwa kama ya ujenzi pia tutaweka kebo”. Ameeleza Mhandisi huyo.
Naye Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi wa mradi huo, Mhandisi Justus Mtolera amesema ujenzi wa bwawa la umeme utakuwa na mashine tisa zenye uwezo wa kuzalisha megawati 235, hivyo kwa pamoja zitazalisha megawati 2,115.