Home VIWANDANISHATI Wawekezaji waomba serikali kuharakisha mradi

Wawekezaji waomba serikali kuharakisha mradi

0 comment 112 views

Kampuni zaidi ya 30 zilizowekeza kwenye sekta ya mafuta zimetoa wito kwa serikali kuharakisha mradi wa uchakataji gesi mkoani Mtwara. Wafanyabiashara hao wametoa kilio hicho walipokutana na Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) jijini Dar es salaam, ikiwa ni muendelezo wa taasisi hiyo kukaa na wadau mbalimbali kujadili changamoto zinazowakabili, kisha kuzifikishwa serikalini ili zipatiwe ufumbuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema moja kati ya changamoto wanayokumbana nayo wawekezaji hao ni mradi huo wa kuchakata gesi asilia kutokuwa na dalili zozote za kuendelezwa. Nyingine ni mikataba ya kazi, usumbufu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mikataba ya makubaliano ya uzalishaji na mauzo kuchukua muda mrefu tangu ichukuliwe na serikali kwa ajili ya kupitiwa upya, pamoja na malimbikizo ya madai ya kodi.

“Tumekutana na sekta ya mafuta na gesi ili kujadili changamoto zao na moja ya changamoto waliyotueleza ni mradi wa kuchakata gesi Mtwara, hivyo tunaomba serikali iuharakishe. Wametueleza kuwa mikataba hii ilichukuliwa na serikali na wao wanalalamika kuwa suala hilo limechukua muda mrefu, hivyo wanaomba kuharakishwa”. Amesema Simbeye.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter