Home VIWANDA Tuzo zatolewa kwa wanafunzi wanasayansi

Tuzo zatolewa kwa wanafunzi wanasayansi

0 comment 107 views
Na Mwandishi wetu

Shirika la Wanasayansi Chipukizi (YST) wametoa tuzo kwa wanafunzi wanasayansi ambao wamebuni bidhaa mbalimbali za kisayansi jijini Dar es salaam. Akiwa kwenye  halfa hiyo, Prof. Simon Msanjila amesema wanafunzi kuendeleza vipaji vyao na kubuni kazi mbalimbali kutaongeza idadi ya wanasayansi nchini.

Ameongeza kuwa huu ni muda muafaka wa kutumia ubunifu wao kwani inajipanga kujenga Tanzania ya Viwanda, hivyo ni faraja kubwa kuona wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi wanabuni vitu vizuri na ameona kuna haja ya kuwasaidia ili kazi zao zifanikiwe kuingia sokoni.

Serikali ikishirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetenga fedha ili kusaidia kazi kama hizi kuingizwa sokoni. Lengo kubwa ni kushawishi vijana wengi zaidi kuongeza ubunifu katika kazi zao. Pia serikali inaangalia uwezekano wa kuwafadhili vijana hawa badala ya kuwapatia mikopo kama ilivyo sasa.

Dk. Gosbert Kamugisha ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa YST amesema tuzo 20 zimetolewa kwa wanafunzi kutoka shule mbalimbali waliofanya vizuri katika ubunifu wao. Mbali na tuzo hizo zawadi nyingine kama kompyuta, fedha taslimu, udhamini wa elimu ya vyuo vikuu na zawadi ya vikombe zimetotelewa. Pia baadhi ya shule wanazosoma wanafunzi hawa zitafanyiwa uboreshaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter