Home VIWANDA Viwanda vingine hatarini kufutiwa umiliki

Viwanda vingine hatarini kufutiwa umiliki

0 comment 102 views
Na Mwandishi wetu

Muda mfupi baada ya serikali kutangaza kufuta umiliki wa viwanda 10 ambavyo wamiliki wameshindwa kuviendeleza, viwanda vingine vipo katika hatari ya kufutiwa umiliki baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhelm Meru kukutana na wamiliki wa viwanda hivyo 11 kwa ajili ya mazngumzo ili kufikia suluhu na kuwapa fursa wenye uwezo wa kuviendesha.

Katibu Mkuu huyo amesema wakati alipokutana na wamiliki hao jijini Dar es salaam kuwa serikali imevumilia vitendo vya kudorora kwa viwanda kwa kipindi kirefu na imefikia maamuzi ya kuvichukua viwanda hivyo na kuruhusu wenye uwezo wa kuvifufua upya kujitokeza ili waviendeleze na kutoa ajira hapa nchini.

Dk. Meru amesisitiza kuwa serikali haijachukua viwanda hivyo ili kuwapa wenye uwezo, bali imeamua kuzungumza moja kwa moja na wamiliki hao ili wapate fursa ya kusema kama wataviendeleza au wameshindwa. Amesema kuwa serikali ni sikivu ndiyo maana wamiliki hao wameitwa na kupewa nafasi ya kujieleza. Ameongeza kuwa lengo kubwa la serikali ni kuvichukua viwanda hivyo na kuwapatia watakaomudu kuvifanya vizalishe na kuongeza mapato.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter