Home VIWANDANISHATI REA yafikia 80% ya vijiji Kilimanjaro

REA yafikia 80% ya vijiji Kilimanjaro

0 comment 133 views
Na Mwandishi wetu

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani amesema asilimia 80 ya vijiji katika Mkoa wa Kilimanjaro tayari vimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akiwa katika sherehe ya uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) ambayo ilifanyika katika kijiji cha Kirya wilayani Mwanga, Dk. Kalemani amesema mpaka kufikia sasa, vijiji 390 kati ya 513 vimeshapatiwa umeme na REA itapeleka nishati hiyo muhimu katika vijiji 123 ambavyo bado havijafikiwa. Mpaka kufikia 2021 vijiji vyote vitakuwa na umeme.

Akizungumzia upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Kalemani amesema mkoa huo unapata kiasi cha megawati 110 japokuwa matumizi yake ni megawati 47, pia amewaomba wananchi wa mkoa huo kutumia umeme kwa shughuli za maendeleo kama vile ujenzi na viwanda.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewapongeza TANESCO na REA kwa kutekeleza mradi huo, amesema umewasaidia wananchi katika vijiji hivyo kujiariri na kuajiriwa katika shughuli mbalimbali zinazotumia nishati hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter