Home BIASHARA Fursa 5 za uwekezaji

Fursa 5 za uwekezaji

0 comment 160 views

Serikali ya Tanzania imekuwa ikiwahamasisha wananchi na raia kutoka nje ya nchi kuwekeza hapa nchini kutokana na uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji. Pamoja na hayo, wamekuwa wakijitahidi kuweka mazingira ya uwekezaji vizuri ili kuendelea kuwavutia wawekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya “Where to Invest in Africa” ya mwaka 2018, Tanzania imeshika nafasi ya 7 kati ya nchi 52 zinazovutia katika sekta ya uwekezaji barani Afrika. Hivyo wawekezaji hawatakiwi kuwa na hofu kuhusu kuwekeza nchini.

Yafuatayo ni maeneo matano ambayo yanavutia kuwekeza Tanzania:

Kukodisha vitu

Kuna vitu ambavyo watu huwa na matumizi navyo kwa siku chache tu na baada ya hapo huwa hawavihitaji tena. Hivyo muwekezaji anaweza kutumia fursa hiyo kuwekeza. Muda mwingine watu hununua vitu na kuvihifadhi kwa sababu hawana matumizi navyo hivyo unaweza kujipatia fedha kupitia vitu ambavyo hutumii au unatumia mara chache.

Kwa mfano unaweza kukodisha magari kwa wananchi wa kawaida au hata wanaotoka nje ya nchi ikiwa huna matumizi na gari hilo na muda mwingine fedha unazozipata kupitia gari moja zinaweza kukupatia mtaji hivyo kukuwezesha kufungua kampuni kubwa ya kukodisha magari. Baadhi ya vitu vingine unavyoweza kukodisha ni nguo, mashine, n.k.

Huduma kwa watalii

Sekta ya utalii ina fursa nyingi za kuwekeza. Hivyo inategemea na mtaji ulionao. Ikiwa huna mtaji unaweza kupata fedha katika sekta hii kwa kuwasaidia watalii katika upande wa lugha ikiwa unajua lugha zaidi ya moja, kwa kuwaonyesha maeneo ikiwa ni mwenyeji. Na kama una mtaji basi unaweza kuwekeza zaidi kwa kufungua kampuni ya kuwahudumia watalii kwa ujumla kwenye usafiri, malazi, muda mwingine mavazi pia. Kwa watu wasio kuwa na mtaji wanaweza kuwasiliana na makampuni makubwa yanayotoa huduma za utalii ili waweze kupata fedha kutokana na uzoefu au utaalamu wao.

Kuagiza na kupokea mizigo

Ikiwa una uwezo wa kuwasiliana na watu wanaoishi nje ya nchi na kutengeneza mtandao wa kutumiwa mizigo kutoka huko na kuituma nchini au kupokea mizigo kutoka huku kwenda katika nchi husika, basi unaweza kuwekeza katika mzunguko huo na kujipatia fedha. Watu wengi wanapenda kuagiza mizigo au kutuma mizigo lakini huwa na hofu kwamba mizigo hiyo inaweza kupotea au kuchelewa kufika na huwa wanataka kampuni au mtu ambaye ni muaminifu na anayeweza kufikisha mizigo kwa wakati. Hivyo ni muhimu kuwa mkweli, muaminifu, na mwenye kujali wateja ikiwa utafikiria kuwekeza katika fursa hii.

Duka la Hardware

Tumezoea kuona maduka ya hardware yana vitu vile vile kila mwaka. Lakini watu hawajui kwamba maisha yanabadilika kila siku na vitu vipya na kwa maumbo tofauti vinatengenezwa, na watanzania kwasababu ya utandawazi na mitandao wanakuwa wanataka kwenda na wakati. Hivyo basi kama mtu ana mtaji anaweza kufanya uchunguzi wa vifaa vya kisasa vya ujenzi, kilimo na vitu vyote vinavoweza kuuzwa katika duka la hardware. Pia inabidi kuwa na watu wa kuwaamini ambao wana uwezo wa kutuma vitu vipya kila vinavyotoka. Ili kukidhi mahitaji ya watu na kuwaondolea ulazima wa watu kuagiza vitu nje ya nchi wakati wana uwezo wa kuvipata ndani ya nchi kwa bei nafuu.

Kusindika chakula

Watanzania ni wazalishaji wa mazao ya chakula na moja kati ya malengo yao ni kupeleka biashara zao kimataifa. Fursa inakuja ni kwamba wengi wao hawana uwezo wa kuzalisha mazao na kuyasindika kwa ajili ya kudafirisha nje ya nchi. Hivyo basi watu wengi wakiwekeza katika hili watapata faida sana na wazalishaji wa chakula watanufaika pia kimaendeleo na kukidhi matakwa ya serikali kukuza sekta ya kilimo na kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.

Fursa ni nyingi hapa nchini, unachohitaji ni kufanya utafiti katika maeneo yanayokuzunguka ili kugundua fursa na kuzifanyia kazi na kujiletea maendeleo. Kwa raia wa kigeni, serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri hususani kwa wawekezaji ili kukuza uchumi wa nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter