Home BENKI CRDB benki yazindua kampeni ya kuweka akiba

CRDB benki yazindua kampeni ya kuweka akiba

0 comment 125 views

Dar es Salaam. Benki ya CRDB imezindua kampeni ya kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.

Kampeni hiyo iloyopewa jina la “Jipe Tano” inalenga kuwasaidia wateja na watanzania kufikia malengo yao ya kimaisha pamoja na kumudu gharama mbalimbali kupitia utamaduni wa kujiwekea akiba.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB Stephen Adili amesema “tuna tambua wateja wetu wana malengo ambayo wamejiwekea katika maisha, na sisi kama benki ya kizalendo tuna jukumu la kuhakikisha wateja wetu wanafikia malengo kupitia huduma na bidhaa bunifu zitolewazo na benki yetu”.

Amesema katika kampeni hiyo, CRDB imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambapo wateja watakuwa wakijishindia zawadi ya Sh 5,000 kila watakapoweka akiba katika akaunti zao ikiwemo akaunti za Watoto Junior Jumbo, Malkia kwa ajili ya wanawake, Schoolar kwa ajili ya wanafunzi, FahariKilimo kwa ajili ya wakulima, Tanzanite kwa ajili ya watanzania waishio nje ya nchi, Pensheni kwa ajili ya wastaafu, na akaunti nyingine za uwekezaji kama Dhahabu, Thamani na akaunti za muda maalum.

Ameeleza kuwa “mteja atakapoweka akiba katika akaunti yake atapata nafasi ya kujishindia Sh. 5,000 kila siku. Tunafanya hivi ili kuongeza hamasa kwa wateja kuweka akiba zaidi na kujenga utamaduni huu kwa watanzania”.

Amesema benki hiyo itakuwa inatoa zaadi kwa washindi 240 kwa siku hadi mwishoni mwa mwezi Desemba kampeni hiyo itakapofika kilele.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Joseline Kamuhanda amesema wateja watahitajika kuweka akiba katika akaunti zao mara kwa mara ili kujiongezea nafasi ya kushinda zaidi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter