Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Rais Samia atangaza mkakati bei ya mafuta

Rais Samia atangaza mkakati bei ya mafuta

0 comment 126 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani ametangaza mkakati wa kubana matumizi ya Serikali katika bajeti ya matumizi ili kupata fedha za kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta nchini.

Ongezeko hilo linalosababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali.

Katika taarifa ya Rais Samia kwa vyombo vya habari Mei 9, 2022 amesema Serikali imesikia kilio cha wananchi cha kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.

“Katika mwaka wa fedha unaoanza Julai mwaka huu tutachukua hatua mbalimbali za kikodi kuweka ahueni kwa wananchi.

“Ndugu wananchi kasi za kupanda kwa bei ya mafuta imetikisa nchi zote duniani, tajiri na maskini, zenye kuzalisha mafuta na zenye kuagiza mafuta, Tanzania kama nchi inayoagiza mafuta haijapona kwenye janga hili.

Serikali imesikia kilio cha wananchi kuhusu ukali wa maisha unatokana na kuongezeka kwa bei ya bidhaaa mbalimbali, ameeleza Rais”.

“Hata hivyo, kutoa nafuu za kupanda kwa bei za mafuta hakuwezi kusubiri hadi mwaka huu wa fedha, nimeamua kwa hiyo wananchi waanze kupata nafuu kuanzia tarehe Mosi Juni.

Nimeelekeza kwamba, Serikali tujibane na tujinyime ili kupata fedha kutoka kwenye matumizi ya kawaida ya Serikali ili ziende kutoa nafuu za bei ya mafuta kuelekea mwaka wa fedha,” amesema Rais Samia.

Vilevile Rais Samia amesema hatua zaidi za kikodi zitatangazwa na Waziri wa fedha katika bajeti ya Serikali mwezi ujao.

“Serikali inatambua adha inayotokana na kupanda kwa bei na hatutasita kuchukua hatua stahiki. Wakati huo huo ni muhimu pia kutambua kwamba yapo matukio ya kidunia yanayosababisha bei kupanda yaliyo nje ya uwezo wetu.

Jambo muhimu hata zaidi ya bei ni upatikanaji wa mafuta yenyewe, bahati nzuri nchini yetu imefanya kazi nzuri kuhakikisha haijakaukiwa na mafuta kama tunavyoona kwenye nchini nyingine, amesema Rais Samia”.

Amewapa pole Watanzania wote kwa kadhia iliyojitokeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter