Soko la uokaji limetajwa kukua kwa kasi na hii inatokana na mtindo wa maisha ya sasa.
Ofisa kutoka Chama cha Waokaji Tanzania (TBA) Simon Chamkali anasema watu wengi wanakula vyakula vya kuokwa hususani keki, mikate na vitafunwa vingine mbalimbali.
“Kazi nyingi na uchovu unawafanya baadhi ya watu kula vitafunwa badala ya mlo kamili, hii imepelekea waokaji kuwa wengi na biashaa hii sasa imepanuka kwa kasi,” anasema Chamkali.
Aidha, kutokana na kupanuka kwa biashara ya uokaji, amewataka waokaji nchini kujisaliji katika Chama hicho ili waweze kutambulika.
“Kwa sasa tuna wanachama takribani 200, natoa wito kwa waokaji wote waje wajisajili,”amesema.
Amesema kwa kujisajili muokaji atapata fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo, kuunganishwa na wateja pamoja na taasisi za fedha kwa ajili ya kukuza mitaji yao.
Amesema lengo ni waokaji wote wawe wamesajiliwa na TBAndani ya miaka mitano ijayo.
Ameeleza kuwa “hii itasaidia kuweka viwango pamoja na bei elekezi kwa bidhaa za uokaji, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imeweka viwango kwa bidhaa mbalimbali lakini wengi wa waokaji hawana huo uelewa”.