Home KILIMOKILIMO BIASHARA Mashamba yaliyotelekezwa miaka 30 kufufuliwa Kilolo

Mashamba yaliyotelekezwa miaka 30 kufufuliwa Kilolo

0 comment 156 views

Bodi ya chai imedhamiria kuyarejesha mashamba ya chai yaliyotekelezwa kwa miaka 30 wilayani Kilolo, mkoani Iringa.

Mkurugenzi wa Bodi ya Chai, Mary Kipeja amebainisha hayo wakati bodi hiyo ilipokutana na wadau wa zao la chai wa Wilaya humo kujadiliana njia bora za kuendeleza zao hilo.

Amesema, mashamba hayo ambayo kwa sasa yanaendelea kusafishwa yataongeza ajira kwa vijana kwa kuwa yatagawiwa kwa wakulima wa chai wilayani humo na wawekezaji.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais , Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha kilimo huku zao la chai likiwa kati ya mazao ya biashara yenye nafasi kubwa katika kuchangia uchumi wa nchi.

Hivyo bodi imejipanga katika kutumia vema fursa zilizopo nakuyafufua mashamba haya ni kati ya mikakati hiyo,” ameeleza Mary.

Wadau hao wamekutana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilolo kwa kushirikisha Uongozi wa Bodi ya Chai, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Peresi Magiri, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Lain Kamendu, Mbunge wa Kilolo Justine Nyamoga pamoja na watendaji wengine wa
wilaya hiyo wanaojihusisha na zao la chai.

Mbunge wa Kilolo Justine Nyamoga amesema kuwa wananchi wapo tayari kutumia fursa zilizopo kwenye zao la chai na uamuzi wa kufufua mashamba hayo utawahamasisha zaidi huku akisisitiza uamuzi huo utaongeza ajira kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya hiyo Peresi Magiri ameihakikishia bodi kuwa wilaya imejipanga kuhakikisha kuwa kila mwenye sifa atapatiwa fursa ya kushiriki kwenye mashamba hayo.

Pamoja na kikao hicho wadau walipata fursa ya kutembelea mashamba ili kuona maendeleo ya mradi wa ufufuaji wa mashamba ambao unatarajiwa kukamilika mapema mwenzi Julai, 2023.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter