Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Waomba serikali kuwakopesha vitendea kazi

Waomba serikali kuwakopesha vitendea kazi

0 comment 123 views

Vitendea kazi vimetajwa kama changamoto inayowakabili wajasiriamali wadogo nchini.

Baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kuangalia namna pia ya kutoa mikopo ya vitendea kazi ikiwemo mashine.

Bahati Malangalila ambae ni mjasiriamali wa kutengeneza vinywaji na vyakula vya lishe ameitaja changamoto hiyo kama kikwazo kikubwa kwa biashara za wajasiriamali kukua.

“Mkopo wa fedha unategemea na ukubwa wa biashara husika, sisi wajasiriamali wengine tunaona ni bora kupewa mkopo wa vitendea kazi kama mashine kuliko mkopo wa fedha ambao ni mdogo na hautoshi kununua baadhi ya mashine,” ameeleza.

Ameeleza kuwa “kwa mfano mimi katika biashara yangu ya uchachushaji, ninatumia njia za asili kabisa, lakini bidhaa hizi ninahitaji kuwa na mashine ya kujaza mvinyo kwenye chupa, kuweka chapa pamoja na kufunika chupa, vyote hivyo ninavifanya kwa mkono.”

Anaeleza kuwa kukosekana kwa mashine kunafanya uzalishaji wa biashara hiyo kuwa wa kusuasua na kuiomba serikali kuangalia jinsi itakavyoweza kuwakopesha mashine wajasiriamali ambao hawawezi kumudu gharama za vitendea kazi.

Fransisca Fransis ambae ni Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake watengeneza batiki Kitende ametoa wito kwa serikali kuangalia namna ya kuongeza mikopo kutoka katika Halmashauri pamoja na kuwakopesha vitendea kazi.

“Kwa sasa tunatoa pesa za marejesho kutoka mifukoni kwa sababu fedha tulizopata zisingeweza kununua mashine na vifaa vingine, tulipewa mkopo wa Sh milioni 15 lakini kwa uhitaji milioni 30 ndio ingetosha,” ameeleza Fransis.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter