Home Elimu Chuo cha Bandari DSM kubadilishana uzoefu na Italy

Chuo cha Bandari DSM kubadilishana uzoefu na Italy

0 comment 198 views

Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Chuo cha Italian Shipping Academy kilichopo nchini Italy ya kubadilishana uzoefu katika mafunzo ya ubaharia na kushirikiana katika tafiti na miradi ya maendeleo ya uchumi wa buluu.

MOU hiyo imesainiwa nchini Italy na Dkt.Tumaini Gurumo, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam na Rais wa Chuo cha Italian Shipping Academy (FAIMM) Eugenio Massolo.

Dkt. Gurumo amesema makubalino hayo ya miaka mitano yatasaidia kuongeza ujuzi kati ya Wanafunzi na Wahadhiri kwa pande zote mbili.

“Nimefurahi sana kuingia Makubaliano haya kwakua wenzetu wapo tayari kushirikiana nasi katika miradi mbalimbali, ninaona ndoto ya kufikia viwango vinavyokubalika na EU inakwenda kutimia,” amesema Dkt. Gurumo.

Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Balozi Tanzania nchini Italy Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Italy nchini Tanzania Marco Lombardi.

Kwa upande wake Balozi Kombo amesema kuwa Italy imepiga hatua katika teknolojia hivyo utayari wao wa kushirikiana na DMI utaiwezesha zaidi Tanzania kukua katika eneo hilo. Vilevile Balozi Kombo ametoa wito kwa pande zote mbili kuteleza vipengele vya makubaliano ipasavyo ili kupata matokeo yanayotarajiwa.

Naye Mkuu wa Chuo cha Italian Shipping Academy Foundation (FAIMM) Eugenio Massolo amesema kuwa makubaliano hayo yatasidia kukuza ujuzi kwa pande zote mbili ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter